TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka
Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha
kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati
akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili
wafawidhi wa serikali wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na
Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa
Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.
Awali
kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na
Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto
zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na
kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za
makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya
kucheleweshwa kwa kesi za hizo.
Kufuatia
kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha
anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka
fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha
Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha
hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa
kazi.
Ametolea
mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili
ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka
inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo
yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
"Oysterbay
pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye
mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu
kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay
likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga
nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment na Polisi wenu
wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa
uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu,
nataka muelewe na muelewe ukweli direction ninayoitaka mimi"
Amesema Rais Magufuli
Aidha,
Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya
kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya
serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na
wanasheria mahiri.
"Niwaombe
mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi
mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na
mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana
na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa
nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa
serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude siku
zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali
inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa
vyovyote serikali inapata kigugumizi"
amesisitiza Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo
zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha
na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa
ujambazi.
Hata
hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka
apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha
vyombo hivyo.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
29
Aprili, 2016
0 comments:
Post a Comment