Thursday, April 28, 2016

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA


>
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.  --- Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini. "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena. Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu. KAWAIDA: Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango. Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima. --- Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini. "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena. Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu. -- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability'' Reply, Reply All or Forward | More Click to Reply, Reply All or Forward
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu