Friday, April 22, 2016


Warembo 14 wajitokeza Miss Tabata 2016
 
Na Mwandishi Wetu
WAREMBO 14 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka malkia wa Tabata mwaka huu ‘Miss Tabata 2016’.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi kila siku kwenye Ukumbi wa Da West Park, ulioko Tabata jijini Dar es Salaam.
Aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Latifa Dibwe (18), Salma Abeid (18), Fatma Mapunda (19), Dinnah David (22) na Joyce Kweka (24).
Wengine ni Neema Makwaia (22), Jesca Daniel (22), Sabrina Kipunga (22) Happiness Mnyeke (20), Grace Matiko (20), Olanda Filima (19),Neema Zablon (21),Joyce Nyimbo (24) na Noela Kyombya (24).
Naye Mkurugenzi wa shindano hilo ambaye pia ni mkuu wa kambi, Godfrey Kalinga alisema kuwa warembo hao wanafundishwa na Neema Mchaki ambaye alikuwa ni mkufunzi wa shindano la Miss Ilala na Miss Tanzania 2014.
Kalinga aliwaomba warembo wengine wenye sifa kujitokeza kushiriki kwenye shindano hilo ambalo huvutia wadau wengi wa sanaa ya urembo nchini.
“Bado tunapokea warembo, tunataka kufanya shindano la kihistoria mwaka huu na tumepanga kuwapeleka washiriki kwenye mbuga za wanyama ili kupromoti utalii wa ndani,” alisema Kalinga.
Aliongeza kuwa washiriki watano watakaoshika nafasi za juu katika shindano hili wataiwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Kanda ya Ilala ‘Miss Ilala’ na baadaye Miss Tanzania.
Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment wakati Ambasia Mallya ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.
Alizitaja kampuni zilizothibitisha kudhamini Miss Tabata kuwa ni CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 na Bob Entertainment.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu