2


SI LA KULIKOSA

Saturday, May 7, 2016

 Watoa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba marehemu Patrick Eleng, baada ya kudondoka uwanjani wakati wa pambano la soka baina ya timu yake Dinamo Bucharest na Viitorul Constanta, usiku wa kuamkia leo Mei 7, 2016 mjini Bucharest Romania
 NA K-VIS MEDIA Na Mashirika ya Habari
MWANASOKA wa Kimataifa wa Cameroun amefariki uwanjani wakati akiichezea timu ya soka ya Romania katika ligi kuu ya nchi hiyo.
Mchezaji huyo Patrick Ekenng alidondoka wakati akiwa uwanjani na timu yake Dinamo Bucharest huku mchezo huo ukionyeshwa Live na TV ya Romania.
Vyombo vya habari vinesema, mchezaji huo mwenye umri wa miaka 26 kutoka nchini Cameroon alipatwa na mshtuko wa moyo na kudondoka kabla ya kukimbizwa Hositali. Msemaji wa Hospitali ya dharura ya Floreasca, Cristian Pandrea amesema madaktari walijaribu kuushtua moyo wake kwa masaa kadhaa lakini ilishindikana.
Msemaji huyo alisema, sababu hasa za kifo chake hazikufahamika
Mchezo huo baina ya Dinamo Bucharest na Viitorul Constanta ulikuwa sare ya mabao 3-3 wakati mchezaji huyo anadondoka uwanjani kiasi cha dakika ya 69.
Ekeng mechezea timu ya taifa ya Cameroon mara mbili, mwaka 2015 kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, timu ya Swiss Club Lausanne, timu ya Hispania ya Cordoba nay a Ufaransa Le Mans.
Marehemu ameacha mke na motto wa kike
Patrick Ekeng enzi za uhai wake wakati akichezea klabu ya Ufaransa

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu