SERIKALI
YAANDAA MPANGO KABAMBE WA MIPANGO MIJI (MASTER PLANS) ILI KUONDOA MIGOGORO YA
ARDHI
Na
Fatma Salum-MAELEZO, Dodoma.
26/5/2016.
Serikali
kupitia
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaandaa Mpango Kabambe
wa Mipango Miji (Master Plan) utakaoainisha matumizi bora ya ardhi na
kuondoa migogoro
ya ardhi nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina
Mabula wakati akijibu maswali ya wabunge
kuhusu mpango wa Serikali kumaliza migogoro ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali
nchini.
Mhe.
Mabula alieleza kuwa Wizara yake inashirikiana na Halmashauri za Wilaya na Miji
18 kwenye program ya Urban Local Government Supporting Programme (ULGSP) katika
kuandaa Mipango Miji hiyo.
Pia
Mhe. Mabula alibainisha kuwa Wizara inaandaa na kukamilisha programu ya kupanga,
kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi Tanzania itakayotekelezwa kwa
kipindi cha miaka kumi kuanzia 2015 hadi 2025.
“Serikali
imekuwa ikiziagiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
upimaji kwa kuwa inatambua umuhimu wa kupima viwanja na mashamba ili kuwa na
matumizi bora ya ardhi yetu” alisema Mabula.
Aidha,
Mabula aliongeza kuwa Serikali kupitia Mradi wa Benki ya Dunia ipo katika
mchakato wa kununua vifaa vya upimaji ambavyo vitasambazwa katika kanda 8 za
Wizara ya Ardhi ili Halmashauri zote zilizopo ndani ya kanda hizo ziweze
kunufaika.
Alieleza
kuwa makadirio ya awali ya gharama za mradi huo ni Dola za Kimarekani Milioni 4
ambapo Dola Milioni 2 zitatumika kwenye upimaji na Dola Milioni 2 zitatumika
kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa.
Katika
kupunguza na kutatua migogoro ya ardhi iliyopo sasa, Mabula alisema kuwa Wizara
ya Ardhi imeandaa kitabu cha orodha ya migogoro nchi nzima kinachoainisha
vyanzo vya migogoro hiyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Hali
kadhalika, Mabula alisema kuwa Wizara imesambaza Sera na Sheria za Ardhi hasa
kwenye maeneo yenye migogoro, wameimairisha mfumo wa kielektroniki katika kutunza kumbukumbu, na kuboresha ofisi
za Kanda ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi.
Mwisho.
|
Home »Unlabelled »
Friday, May 27, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment