Thursday, June 16, 2016


AZANIA BANK YAKABIDHI MADAWATI 50 SHULE YA MSINGI MNAZI MJINI MOSHI. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akizungumza wakati wa kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi katika manispaa ya Moshi ikiwa ni kuunga mkono agizo la rais John Magufuli la kupunguza tatizo la Madawati kwa shule za msingi.
Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi,Hajira Mmambe akizungungumza juu ya hatua ya benki hiyo kuunga mkono agizo la rais John Magufuli la kutatua tatizo la Madawati kwa shule za msingi nchini. 
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Madawati 50 yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi wakifuatilia hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Deodatus Nyoni akizungumzia juu ya upungufu wa Madawati 701 ulipo sasa kwa shule za msingi na Sekondari.
Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi, Hajira Mmambe akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky Madawati yaliyotolewa na benki hiyo. Wengine ni wanafunzi wa shule ya msingi Mnazi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadicky (katikati) akiwa ameketi kwenye moja ya Madawati yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa shule ya msingi Mnazi, kulia ni mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga na kushoto ni meneja wa Azania benki tawi la Moshi, Hajira Mmambe. 
Wanafunzi katika shule ya msingi Mnazi wakiwa wamekaa katika Madawati yaliyotolewa na benki ya Azania tawi la Moshi. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadicky, akisalimiana na wanafunzi katika shule hiyo.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi, Raymond Mboya akitoa neno la shukrani mara baada ya kupata msaada wa Madawati kutoka Benki ya Azania tawi la Moshi. 
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi, Raymond Mboya akiteta jambo na Meneja wa benki ya Azania tawi la Moshi, Hajira Mmambe wakati wa hafla ya kukabidhi wa Madawati kwa shule ya msingi Mnazi. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadicky akisalimiana na wafanyakazi wa benki ya Azania tawi la Moshi pamoja na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog kanda ya kaskazini.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu