Thursday, June 30, 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).  Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya kufanya uteuzi huo.  Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri - Sanaa (M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.

Imetolewa na,
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu