Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Mabasi
Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), David Mgwasa (kushoto),akionesha
kipeperushi chenye maelezo ya matumizi ya kadi zitakazotumika katika
mabasi hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya
Udart Jangwani jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya
kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi
ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano
huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabar ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini
Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi
maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa
alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao
na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya
kuondoka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo,
Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000
ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi
moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja
wao.
"Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya
nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo
zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na
kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu
Aliongeza kuwa katika nchi nyingi
zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa
nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya
kuzoeleka.
Alisema licha ya kuanzisha huduma ya
kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya
kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#
0 comments:
Post a Comment