Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia kitabu cha Binti Foundation wakati wa Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs
iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo
aliahidi kuwasomesha watoto 100 na aliwasihi Wanawake wanapoweka
mipango ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kulia) akiwa pamoja na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa mara baada
ya uzinduzi wa Binti Clubs jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha
Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs iliyoandaliwa na taasisi
isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye Tamasha Fadhili Mtoto Asome pamoja na Binti Clubs
iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Binti Foundation ambapo
aliahidi kuwasomesha watoto 100 na aliwasihi Wanawake wanapoweka
mipango ya kimaendeleo kuwashirikisha pia wanaume
Sehemu ya watoto walioshiriki kuonyesha mitindo mbali mbali ya Mavazi pamoja na Wabunifu wao.
NA MWANDISHI WETU
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan, amekubali kuwa mlezi wa mlezi wa Binti
Foundation na pia ametoa ahadi ya kusomesha watoto 100. Mke wa Waziri
Mkuu, Mary Majaliwa naye ametoa ahadi ya kusomesha watoto 50.
Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati hafla ya uzinduzi wa Binti club iliyofanyika sambamba na harambee ya fadhili mtoto asome ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto 500 wa wilaya ya Kinondoni iliyoandaliwa na Shirika lisislo la Kiserikali la Binti Foundation katika ukumbi wa jengo la Jubilee Towers linalomikiwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF jijini Dar es salaam.
Pia ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yanayoshughulikia masuala ya wanawake na watoto kujenga utamaduni wa kushirikisha wanaume katika kampeni za kumwinua mtoto wa kike kwa lengo la kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.

Alisema wanaume kama wakala
wa mabadiliko wanapaswa kushirikishwa na wajue ajenda ili wawe mabalozi wazuri katika
kuzungumzia umuhimu wa kumwinua mtoto wa kike kielimu, kiafya na kwenye masuala
ya ujasiriamali.
"Tuwaingize wanaume
kama wakala wa mabadiliko, tuwashirikishe, wajue ajenda zetu katika mapambano
hayo. wanaume wanashikilia sehemu nyingi, watumie nafasi hizo tulete mabadiliko,"
alisema Makamu wa Rais na kuongeza
"Penye mkusanyiko wa
watu 100, ukiingiza wanaume 20, na wakajua madhumuni ya mkusanyiko wetu,
wataenda kushawishi wenzao 20,000 huko nje."
Aliipongeza Taasisi hiyo ya
Binti Foundation kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu
kwani safari ya mtoto wa kike ya kupata elimu inakuwa na ugumu zaidi kuliko
wanaume kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mila
potofu, hali ya uchumi katika familia na jinsi jamii inavyomwangalia kutokana
na ujanajike wake.
"Tuna kazi kubwa ya
kumtayarisha mtoto wa kike aweze kupambana na changamoto zinazomzunguka,"
alidokeza.
Mheshimiwa Samia alitumia
fursa hiyo kuelezea hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali katika
kukabiliana na changamoto za elimu ikiwa ni pamoja na kuondoa ada katika shule
za msingi na sekondari, kuboresha ajira za walimu pamoja na maslahi yao,
kujenga mabweni kwa wasichana na kuondoa tatizo la madawati ambapo amewashukuru
Watanzania kwa kuchangia madawati.
Aliwataka wazazi kuwatunza
watoto wao kwani ni zawadi kutoka kwa Mungu na kuhakikisha wanapata elimu zote
ya dini na ya dunia ili kuwajenga kimaadili waweze kuwa raia wema.
Mtendaji Mkuu wa Binti
Foundation Johari Sadik alimweleza Makamu wa Rais kuwa shirika hilo liliamua
kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwawezesha watoto kumudu masomo yao na
hatimaye kufikia malengo yao.
"Kwa hiyo ukiwa na
fedha taslimu, ama vifaa kama vile kalamu, madaftari, pedi, vyote tunapokea kwa
ajili ya kusaidia watoto ambao malengo yao yanaweza yasitimie kutokana na
changamoto hizo,"
Kampeni hiyo ya fadhili mtoto asome imeanzia kwa watoto 500 wanaoishi kwenye mazingira magumu wa shule za msingi Mwananyamala, Hananasif, Kumbukumbu na Msasani zilizoko katika wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment