2


SI LA KULIKOSA

Monday, June 27, 2016

MAKAMU WA RAIS KATIKA TAFRIJA YA FUTARI ILIYOANDALIWA NA BAKWATA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania  (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir akizungumza wakati wa tafrija ya futari iliyoandaliwa  na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania ambapo alisema uongozi wa sasa wa BAKWATA umedhamiria kudumisha umoja,upendo na mshikamano baina ya Waislamu wote nchini, Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri  Muungano wa Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Shekh Alhad Mussa Salum akitoa utambulisho wa wageni wa jumuiya mbali mbali za waislam waliohudhuria tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Wanawake nchini Bi. Shamim Khan wakati wa tafrija ya futari liyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Kindondoni Muslim. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu