Friday, June 10, 2016



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi, akisaidiana na Mwenyekiti wa Banki ya Diamond Trust (DTB), Bw. Abdul Samji, kukata utepe katika uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo la CBD. Kushoto ni Bi. Nasim Devji Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo nchini, kulia ni Mwakilishi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Hezron Gyimri. Tawi la CBD linakuwa ni tawi la 25 la benki hiyo nchini Tanzania na la 11 jijini Dar es Salaam.

Na Imma Matukio Blog

Benki ya Diamond Trust Tanzania, (DTB Tanzania),leo imezindua rasmi tawi la CBD lilipolo katikati ya jiji la Dar es Salaam kwenye jengo la Diamond Plaza, makutano ya barabara ya Samora na mtaa wa Mirambo. Tawi la CBD ni la ishirini na tano nchini na la kumi na moja katika jiji la Dar es Salaam.

Tawi la CBD litafunguliwa jumatatu hadi ijumaa, saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni na Jumamosi saa 3:30 asubuhi hadi sa 7:00 mchana.

Akihutubia katika hafla fupi iliyofanyika ndani ya benki, Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Raymond Mushi, alitoa pongezi kwa uongozi wa benki ya DTB Tanzania kwa ufunguzi wa takriban matawi mawili kila mwaka licha ya changamoto zinazokabili sekta ya fedha nchini na duniani kwa ujumla. Benki ya DTB imefanikiwa kufungua matawi ishirini na moja katika miji kumi na tatu ndani ya mika minane (2007 – 2016).

“Ninawapongeza na kuwashukuru kwa jitihada zenu za kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi na kuwajenga watanzania kiuchumi. Enzi za kusafiri masaa kwenda kwenye benki na kisha kupanga foleni kwa muda mrefu kwa ajili ya kupata huduma za kibenki imeshapita” Ndugugu Mushi iliongeza.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Ndugu Abdul Samji, alitoa pongezi kwa menejimenti ya Benki kwa matokeo bora ya biashara ya kwa mwaka uliopita 2015, ambapo Benki ilitangaza mafanikio makubwa katika matokeo ya biashara.

“katika ripoti hiyo, akiba za wateja zilikukua kwa asilimia 26.8% kutoka shilingi bilioni 581 mwaka 2014 hadi shilingi bilioni 737 mwaka 2015. Aidha, kulingana na ripoti za mabenki zilizotolewa kwa mwaka 2015, DTB ni benki ya sita kwa ukubwa wa amana za wateja nchini. Benki ya DTB Tanzania pia inashikilia nafasi ya 4 katika viwango vya faida katika matokeo ya biashara ya miezi mitatu ya kwanza mwaka huu.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa faida kabla ya kodi mwaka 2015 ilikuwa shilingi bilioni 27.33 sawa na ongezeko la asilimia 36.03% ikilinganishwa na shilingi bilioni 20.1 mwaka 2014. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa DTB inakua kwa kasi ukilinganishwa na ukuaji katika sekta ya kibenki nchimni.

DTB Tanzania ina matawi 25 nchini, ikiwa na matawi kumi na moja (11) jijini Dar es Salaam (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, barabara ya Nyerere, Msimbazi - Kariakoo, barbara ya Nelson Mandela, Upanga katika barabara ya umoja wa mataifa na katika makutano ya barabara ya Mirambo na mtaa wa Samora). Vile vile ina matawi katika miji ya Arusha (2), Mwanza (2) na katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora , Tanga na Zanzibar.

DTB Tanzania ni mshirika wa mtandao wa maendeleo ya kiuchumi wa Aga Khan - Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) ambao ni sehemu ya mtandao wa maendeleo wa Aga Khan Development Network). DTB Kenya ni miongoni mwa wanahisa muhimu wa DTB Tanzania.



DTB Tanzania pia ni sehemu ya mtandao wa wa mabenki ya DTB Group yenye matawi zaidi ya 120 Afrika Mashariki katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi.


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu