Na Mwandishi wetu Washington
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha
Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad, jana alimaliza ziara yake
nchini Marekani iliyochukua muda wa wiki moja.
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), maalim Seif Sharif Hamad (Picha na http://swahilivilla.blogspot.com/)
Maalim Seif alikhitimisha ziara yake hiyo kwa mkutano wa hadhara ambapo
alipata nafasi ya kuongea na Watanzania waishio nchini humu.
Katika Mkutano huo, mwanasiasa huyo gwiji nchini Tanzania alisema kuwa
lengo la ziara yake ni kuuelezea ulimwengu kukhusu kile kilichotokea
Zanzibar kufuatia uchaguzi wa Oktoba 25 na mwelekeo wa demokrasia nchini
Tanzania kwa ujumla.
Aliielezea ziara yake hiyo nchini Marekani kuwa imezaa matrunda. “Sina
budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa tumeeleweka na ziara yetu imezaa
matunda” alisema Maalim Seif.
Sehemu ya hadhira wakimsikiliza kwa makini Maalim Seif
Kukhusiana na zoezi la uchaguzi wa mwaka jana Visiwani Zanzibar, Maalim
Seif alisema kuwa, uchaguzi huo ulihudhuriwa na waangalizi wa Kimataifa
na wa ndani kutoka pande zote za Muungano, Bara na Zanzibar, na
wachunguzi wote hao walithibitisha kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa
haki. “Waangalizi wote, wote kabisa, walikiri kuwa uchaguzi ulikuwa huru
na wa haki”, alisisitiza kiongozi huyo na kuongeza kuwa “Ulikuwa
uchaguzi bora kabisa kuliko chaguzi zote zilizotangulia Zanzibar”
0 comments:
Post a Comment