2


SI LA KULIKOSA

Sunday, June 19, 2016


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, (kushoto), akimbeba motto aliyepewa jina lake (Tulia), wakati alipofika hospitalini kumpongeza mama mzazi wa motto huyo, Bi. Mariam Abdallah Ulege, mke wa mbunge wa Mkuranga Mh. Abdallah Ulehe. Hatua ya Dkt. Ackson inafuatia maelezo ya mbunge huyo aliyoyatoa bungeni mjini Dodoma akimshukuru na kumpongeza mkewe kwa kumzaa motto huyo wa kike na kumsifia kuwa mkewe hakukatab tama licha ya kujifungua mara mbili watoto lakini kila motto alipofikia umri wa miezi 9 alifariki dunia.

 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulege (kulia), akimtambulisha Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson (wapili kulia), kwa viongozi wa jimbo la Mkuranga, wakati alipofika Hospitali ya Taifa Muhimbili, kumpongeza mke wa mbunge huyo Bi. Mariam, kwa kujifungua mtoto wa kike aliyepewa jina la Tulia
  Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto wa mbunge wa Mkuranga  aitwae Tulia Abdallah Ulega  katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson akielekea wodini kumuona mtoto Tulia 


 Naibu Spika akimkabidhi zawadi za mtoto Tulia, mhudunu wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
 Naibu Spika akizunguzma na waandishi wa habari mara baada ya kumpongeza mzazi
Naibu Spika akipokewa na mbunge Ulege
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu