Mratibu wa Shindano la Dance 100% 2016,
Brendansia Kileo(kushoto)na Jaji wa shindano hilo,Khalila
Kells(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu(katikati) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo(hawapo pichani)wakati wa kutangaza Uzinduzi na
Udhamini wa shindano hilo litakaloanza tarehe 16 mwezi huu, Kundi litakaloibuka
mshindi wa shindano hilo litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano
hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania pamoja na
Coco-Cola.
Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiteta jambo na majaji wa shindano la Dance
100% 2016,Super Nyamwela(katikati)na Khalila Kells,Wakati wa kutangaza
Uzinduzi na Udhamini wa shindano hilo leo jijini Dar es Salaam,
litakaloanza tarehe 16 mwezi huu, Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo
litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV
na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania pamoja na Coco-Cola
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi na Udhamini wa shindano la Dance 100%2016 jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2016, litakaloanza tarehe 16 mwezi huu, Kundi litakaloibuka mshindi wa shindano hilo litaondoka na kitita cha shilingi Milioni 7. Shindano hilo linaandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania pamoja na Coco-Cola.
NA K-VIS MEDIA
MASHINDANO
ya kucheza muziki ya vijana maarufu kama Dance 100%
yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV)
yanatarajiwa kuanza Julai 16 mwaka katika viwanja mbalimbali jijini Da r es
Salaam. Yakitangazwa wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam ambapo Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza kuendelea kudhamini mashindano
hayo.
Akiongea
na waandishi wa habari,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikidhamini mashindano hayo kwa kipindi cha
miaka minne mfululizo na katika msimu wa mwaka huu imejidhatiti kwa kuweza
kuendeleza gurudumu la tasnia hii.
Nkurlu
alisema kuwa Vodacom imeendelea kudhamni shindano kwa kutambua kuwa muziki na
michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua
kimaisha.
Aliongeza
kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa
nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo
makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari
wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia
nyanja mbalimbali ikiwemo michezo, burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa
na kampuni hiyo.
“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza
kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo
tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki
wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi
kujiajiri kupitia katika sanaa”Alisema Nkurlu.
Aliwataka vijana
waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze
kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia
nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia
michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele
kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
Naye
Mratibu wa Shindano hilo kutoka kituo cha televisheni cha Afrika Mashariki
‘Brendansia Kileo alisema kuwa mashindano haya kwa msimu wa mwaka huu
yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania na kampuni ya Coca-Cola kama kinywaji rasmi
cha Dance 100% 2016. Mashindano haya yataanza kufanyika jijini Dar es
Salaam katika viwanja vya leaders club, mashindano yataanza na raundi tatu za
usaili tarehe 16,23 na 30 Julai (2016) na kufuatia hatua za robo na nusu
fainali na kasha Fainali. Aliyataka makundi ya dansi kujitokeza kujiandikisha
kushiriki,Pia alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kushuhudia
michuano ya usaili “LIVE’ bila kiingilio chochote.
“Huu ni mwaka wa
Tano (5) East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya na mara ya nne
(4) chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya
yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya
nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki na washindi wakiwa vinara
wakutangaza Dansi katika nchi mbali mbali kama T- Africa, The Chocolate, Wakali
sisi na WD”Alisema Kileo
Alisema kuwa
mashindano hayo yatakuwa yanafanyika wikiendi kwa muda wa miezi mitatu vilevile
yatakuwa
yakionyeshwa na
kituo cha televisheni cha East Afrika kila Jumapili saa moja kamili usiku
na kundi litakaloibuka na ushindi litajinyakulia kitita cha shilingi
Milioni saba (7) na mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi milioni
(2) na mshindi wa tatu atapongezwa na shilingi milioni mmoja (1) tofauti na
miaka ya nyuma.
0 comments:
Post a Comment