Wednesday, July 13, 2016



NA SHAMIMU NYAKI WHUSM
SERIKALI kupitia Jeshi la polisi limewaasa vijana nchini kushiriki katika michezo mbalimbali ya kuigiza yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupambana na kuzuia uhalifu.

Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Inspekta Salum Abdalah (pichani juu), kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi alipokuwa akitoa mafunzo kwa vijana kuhusu Umuhimu wa kutoa elimu kuhusu kuzuia na kupambana na uhalifu nchini kupitia michezo ya kuigiza.

Inspekta Salum amesema kuwa miongoni mwa mikakati ya serikali ni kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na tabia njema na kupata kipato cha halali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya stadi za kazi kwa lengo la kuimarisha na kukuza uchumi, pamoja na kuwapa uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.
“Ili kuwawezesha vijana kuwa na tabia njema na kuwa na maadili yanayotakiwa hatuna budi  kuanzisha mbinu za kuwawezesha kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, ulinzi shirikishi na kuwepo kwa mipango thabiti wa kushiriki katika mafunzo, semina na warsha mbalimbali”. Alisema Inspekta Salum.
Inspekta Salum ameongeza kuwa wananchi ,wadau pamoja na mamlaka zinazohusika na maendeleo ya Vijana, Michezo na ujasiriamali kuwahamasisha vijana  ili waweze kujshughulisha na  shughuli zinazoleta maendeleo kwa taifa na kujiepusha katika vitendo vya uhalifu.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Bw Ismael Mnikite  amesema mafunzo hayo yamemuwezesha kuelewa umuhimu wa ulinzi shirikishi  kwa vijana kwakua anaamini  ndio wenye uwezo mkubwa wa kushawishi jamii kujiepusha na vitendo viovu.
“Mafunzo haya yameniwezesha kuelewa umuhimu wa kuwa mfano  kwa jamii kwani nitatumia elimu hii kupanua uwezo wa kutafuta miradi itakayoniwezesha kupata mikopo  kutoka kwa wawezeshaji ili nisipate tamaa ya kujiingiza katika uhalifu”.Alisema Bw. Ismael.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana ili kuwasaidia vijana kuwa raia wema na kushiriki ipasavyo katika shughuli za ujasiriamali na ulinzi wa jamii kwa kutumia elimu na vipaji walivyonavyo.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akitoa mada kuhusu umuhimu wa sekta ya filamu kwa vijana katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana kuhusu vijana kujiajiri kupitia sekta ya filamu Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Bibi. Venorose Mtenga akizungumza na vijana kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Hafidhi Omary akichangia mada katika mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.


Zuhura Madaba akichangia mada katika mafunzo kuhusu umuhimu wa kujiajiri kupitia ujasiliamali na filamu katika mafunzo yaliyoandaliwa na Idara ya Maendeleo ya Vijana Julai 12, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu