Wednesday, July 13, 2016

JINSI YA KUFIKA NA KUFURAHIA MAISHA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA

Barabara ya kupita Igagala katika wilaya ya Uvinza ndiyo kwa sasa inatumika kusafirisha watalii wanao elekea Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika .
Safari kwa njia ya barabara huishia katika kijiji cha Rukoma kilichopo katika wilaya ya Uvinza ambapo wageni hulazimika kutumia usafiri wa boti kupitia Ziwa Tanganyika.
Safarini ya kwenye maji huchukua Dakika 60 hadi 90 kufika katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ambayo inasifika kwa utalii wa Sokwe Mtu.
Njia nyingine ya kufika katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ni kwa kutumia usafiri wa anga ambapo ndege ndogo zimekua zikifanya safari ya kufikisha watalii katika hifadhi hiyo.
Unapofika katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,eneo mojawapo la kupumzika ni eneo linalojulikana kama Mango Tree Bandas ambako wageni wanapata sehemu ya kupumzika kwa gharama nafuu.
Njia za kuelekea katika nyumba maalumu kwa ajili ya mapumziko.
Moja ya jengo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ambalo linatumika kama Restaurant.
Bandas ambazo zimekuwa zikitumika kupokea wageni wanaofika katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale .
Sehemu ya ndani ya nyumba hizo .
Sehemu za Maliwato na Bafu ndani ya nyumba hizo.
Mbali na eneo hilo pia zipo Hteli za Kitalii ndani ya Hifadhi ya TAifa ya Milima ya Mahale ,mojawapo ni Nomad Lodge.
Sehemu ya kupumzika wageni katika Hotel ya Kitalii ya Nomad Lodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.
Eneo hili hutumiwa na wageni kwa ajili ya kutizama jua linavyozama pamoja na kufurahia mandhari ya ziwa Tanganyika.
Muonekano wa Vyumba vya kulala katika Hoteli kitalii ya Nomad Lodge.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog ,aliyekua Kigoma.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu