Thursday, July 14, 2016

KAMPUNI YA KANJI LALJI YATOZWA FAINEI YA SHILINGI MILINI ISHIRINI NA LAKI TANO



Naibu Waziri wa Osi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh,Luhaga Mpina akipata maelezo
kutoka kwa uongozi wa kiwanda cha bia serenge) alipofanya ziara ya kukagua Mazingira ka)ka eneo hilo
la viwanda linalotuhumiwa kuchafua mazingira.

Naibu waziri Osi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh, Luhaga Mpina akipata maelezo
kutoka kwa mbunge wa temeke mh,Abdallah Mtolea kuhusu uchafuzi wa mazingira wilaya ya temeke
 
 
 
 


  • EVELYN MKOKOI
    AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
    DAR ES SALAAM
    14/7/2016Kampuni ya usarishaji ya Kanji Lalji iliyopo mtaa wa Serenge wilayani Temeke jijini Dar es
    Salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na laki tano, na kutakiwa kulipa faini hiyo ndani
    ya siku saba, kwa kosa la kuririsha maji yenye sumu kaka mitaro ya maji ya mvua inayoelekea
    kwenye makazi ya watu na mazingira na hivyo kuhatarisha maisha na afya za viumbe hai.
    Naibu Waziri Osi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ametoa kauli hiyo leo kupia
    Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira NEMC kaka ziara yake ya kukagua viwanda na usa wa
    mazingira jijini dar es salaam.
    Ziara hiyo ya Naibu waziri Mpina, iliyopelekea naibu waziri huyo kuinuka Osini na kufanya
    ukaguzi wa kushtukiza kaka baadhi ya viwanda hivyo, imetokana na malalamiko ya baadhi ya
    wanachi kaka maeneo husika hususan wenye viwanda.
    Naibu waziri mpina amesema kuwa kutozwa faini ni hatua ya pili kwa baadhi ya viwanda baada
    ya kupewa onyo na maelekezo na NEMC na manispaa, na aliongeza kuwa kwa kutokui taasisi
    za serikali baada ya adhabu hii hatua itakayofuata ni ya kuvifungia viwanda hivyo.
    Kwa upande mwingine Mhe. Mpina amekipongeza kiwanda cha Serenge breweries kwa kui
    kauli ya serikali kwa kulipa faini iliyotozwa awali ya kiasi cha shilingi milioni kumi na sita kwa
    kosa la uchafuzi wa mazingira na kuwashukuru wakazi wanaozunguka kiwanda cha SBL pamoja
    na Mbunge wa TEMEME (CUF) Mhe.Abdallah Mtolea kwa kutoa taarifa za uchafuzi wa mazingira
    na kukipa kiwanda hicho siku 45 kufanya marekebisho madogo madogo ya kimazingira
    kiwandani hapo.
    Aidha, Adhabu nyingine ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira imetolewa kwa wamiliki wa eneo
    la kampuni ya CI group, ambao ni Prime Liberty Limited ya kutakiwa kulipa faini ya shilingi
    milioni 15 kwa muda wa siku saba, na kufanya jumla ya faini za uchafuzi wa mazingira
    zilizotozwa kwa siku ya leo kuwa shilingi milioni 39 na laki tano
mapema hii leo

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu