Friday, July 22, 2016

MISS CHANGOMBE KUFANYIKA LEO IJUMAA

Na Peter Mwenda
WAREMBO 15 wanaingia kilingeni kumtafuta mrembo wa Chang/ombe Miss Chang'ombe katika mashindano yanayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa yatakayofanyika ukumbi wa TCC Sigara.
Mratibu wa Mashindano hayo, Gervas Sinkala alisema jana kuwa maandalizi wa mashindano hayo yamekamilika na warembo wote wamejiandaa vya kutosha kuwani taji hilo.
Alisema mrembo watakaowania taji hilo ni Anita Medard, Prisca Sarakikya, Diana Joseph, Leah Hamad, Zuhura mohamed,Shani Mshamu, Hadija Masoud, Zahara Msangi na Devotha Benard.
Wengine ni Nancy Mushi, Irene Bega, Sharifa Said, Jesca Nassari, na Sabrina Ramadhani ambao washindi watatu wa kwanza watazawadiwa zawadi nono na kupewa nafasi ya kusoma kozi katika chuo  cha DATASTAR Training .
Alisaema mashindano hayo yatafuatiwa na burudani ya muziki kutoka katika bendi ambayo alisema itatambulkishwa kumbini hapo
mwisho
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu