Na Mwandishi
Wetu
SHINDANO la
kumsaka Miss Tabata 2016 litafanyika Julai 22 kwenye Ukumbi wa Da West Park,
Tabata.
Mratibu wa
shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa warembo 38 wanaendelea na
mazoezi kujiandaa na shindano hilo linaloandaliwa na Keen Arts na Bob
Entertainment.
Kapinga alisema
kuwa watafanya mchujo na kubaki na warembo 16 tu watakaopanda jukwaani.
Warembo
wanaoendelea na mazoezi chini ya wakufunzi Neema Mchaki, Bokilo na Pasilida
Bandali ni Happiness Paul (21), Neema Makwaia (21), Rose Lucas (22), Mariam Maabadi
23), Sabrina Khalifa (20), Catherine Alex (22) na Grace Malikita (21).
Wengine ni
Rachel George (21), Nasra Munna (23), Jackline Evarest (21), Flora Msigwa (21),
Akiza Mugashe (21), Neena Linus (21), Noela Pastory (21), Neema Zablon
(24), Narcisa Wilbert (19) na Jesca
Jackson (22).
Pia wamo Latipha Dibwe (18), Salma Abeid (19),
Fatma Mapunda (22), Dinnah David (24), Joyce Kweka (22), Jesca Daniel (22), Happiness Mnyeke (20), Grace Matiko (19), Olanda Lifilima (21),
Joyce Nyimbo (23), Zena Bakari (17), Sylvia Weru (20), Esther Ikwabe (20), Tamika
Mwakitalu (23), Fides Fredson (22), Sharifa Ally (23), Monica Massory (21),
Veronica Godfrey (21) na Rahma Huwel (24).
Naye Mkurugenzi
wa shindano hilo ambaye pia ni mkuu wa kambi, Godfrey Kalinga alisema warembo
watakaoshiriki kwenye fainali watatembelea mbuga za wanyama ili kupromoti
utalii wa ndani. Alisema, washiriki watano watakaoshika nafasi za juu
watashiriki kwenye shindano la Kanda ya Ilala ‘Miss Ilala’, na baadaye Miss
Tanzania.
Miss Tabata
inaandaliwa na Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment wakati Ambasia
Mallya ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.
Miss Tabata
inadhaminiwa na Lete Raha, DataStar College, Global Publishers, CXC Africa,
Fredito Entertainment, Saluti5 Kitwe General Traders na Bob Entertainment.
Baadhi ya
warembo wanaoshiriki Miss Tabata 2016 wakiwa kwenye pozi.
|
0 comments:
Post a Comment