Monday, July 18, 2016



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , paul Makonda akizungumza ndani ya Power Breakfast ya Clouds Fm


Na Mwandishiwetu, Dar es Salaam
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwavulia uvivu wale wote wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.

Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kuelza maswala kadhaa yausuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina lake.
“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inanza na cheo changu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda sio vingine hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda.
Anasema kuwa juu ya agizo batili lililopostiwa katika mitandao ya kijami kuwa wasiokuwa nakazi kwamaba watakwenda jela sio la account yake bali yeye ameagiza wenyeviti wa serikali ya mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.
Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe ataocha kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga.

Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huu kuwa makini na kufata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa.
mwisho



Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu