Waziri
Mkuu wa Israeli, Benjamin Bibi Netanyahu, (katikati), akitabulishwa na
mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Waziri wa Mambo ya Nje
wa Tanzania, Balozi Augustin Mahiga, (kushoto)na Rais wa Rwanda, Paul
Kagame (kulia), Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Ethiopia
Hailemariam
Desalegn, kwenye Ikulu ya Naklasero nchini Uganda.
NA K-VIS MEDIA/NA
MASHIRIKAYA HABARI
Waziri Mkuu wa Israeli,
Benjamin Bibi Netanyahu, amekuwa ni kiongozi wa kwanza wa juu wa serikali ya
nchi hiyo aliyeko madarakani kutembelea barani Afrika, tangu Yitzhak Rabin,
aliyepata kuwa waziri Mkuu wan chi hiyo amtembelee Mfalme Hassan II wa Morocco,
mnamo mwaka 1993.
Kituo cha kwanza cha
Netanyahu kutembelea Afrika iliku Uganda, akaenda Kenya, na kumaliziana
Ethiopia.
Akiwa Uganda, Netanyahu alifanya
mkutano na baadhi ya viongozi wa nchi za Kiafrika kutoka Sudan Kusini,
Tanzania, iliyowakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa,
Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga, na Zambia.
Hata hivyo pamoja na mkutano
huo na viongozi wa kiafrika nchini Uganda, vyombo vya habari havikuutilia
maanani zaidi mkutano huo na badala yake viliangazia zaidi tukio la kuzindua mnara
wa kumbukumbu ya miaka 40 ya operesheni ya kijeshi iliyofanywa na Makomandoo wa
Israeli wakati wakiokoa mateka raia wa Israeli kwenye uwanja wa ndege wa Entebe
mnamo mwaka 1976.
Katika operesheni hiyo ya
aina yake, kiongozi wa makomandoo hao, Yonatan Bibi Netanyahu, kaka wa Waziri
Mkuu Benjamin Netanyahu, aliuawa.
Israeli ililazimika kutuma
makomandoo wake kuokoa raia wake waliotekwa nyara wakiwa ndani ya ndege ya shirika
la ndegge la Ufaransa (Air France). Ndege hiyo ilitekwa nyara na wanamgambo wa
Kipalestina, dakika 15 baada ya kuruka kutoka uwanja wa nege wa Tel-Aviv nchini
Israel ikielekea Paris Ufaransa.
Wanamgambo hao wa
Kipalestina, walifanya tukio hilo wakishinikiza wenzao waliokuwa wakizuiliwa
kwenye magereZa nchini Israeli waachiliwe.
Tukio la kuuawa kwa Kakak wa
Waziri Mkuu wa Israeli, ndio lililomsukuma kiongozi huyo kuingia kwenye siasa.
Hata hivyo mataifa mengi ya
kiafrika hususan kusini mwa jangwa la Sahara, yalijuwa hayaiungi mkono Israeli
kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya Wapalestina.
Ukiacha Uganda, Netanyahu alikwenda Kenya,
ambako enzi za utawala wa Kenyatta, Israeli ilikuwa swahiba wake, na hata
Netanyahu akisalimiana na Balozi Mahiga
Netanyahu (kushoto0, na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegn
Netanyahu akiwa na Rais Museveni kwenye uwanja wa Entebe nchinihumo
Netanyahu akiweka shada la maua kwenye mnara huo wa kumbukumbu
Netanyahu akikagua gwaride la askari polisi nchini Kenya
Netanyahu akikagua gwaride uwanja wa ndege wa Entebe nchini Uganda
Netanyahu akiwa na Rais Uhuru Kenyatta, Ikulu ya Nairobi
Netanyahu akiteta jambo na mwenyeji wake, Rais wa Rwanda, Paul Kagame mjini Kigali |
Kiongozi wa operesheni ya kuokoa mateka wa Israeli, Komandoo Yonatan Bibi Netanyahu. Kaka wa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Bibi Netanyahu. Kiongozi huyo aliuawa kwenye harakati za kuokoa mateka |
0 comments:
Post a Comment