Mgeni
rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli.
Waendesha baiskeli kutoka mikoa
sita ya kanda ya Ziwa wakijiandaa kuchuana wakati wa Mashindano ya mbio za baiskeli ya Acacia Tufankiwe
Pamoja Cycle Challenge 2016 yaliyofanyika mkoani Shinyanga chini ya yakidhaminiwa
na kampuni ya Madini ya Acacia .
Baadhi ya
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe
Pamoja Cycle Challange 2016 wakitafakari kabla ya kuanza kwa mbio
hizo.
Meneja
Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo akizungumza jambo na Mgeni Rasmi
,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura
kabla ya kuanza kwa mashindano ya mbio za Baiskeli.
Mwenyekiti
wa chama cha mchezo wa Baiskeli Tanzania (CHABATA) Godfrey Mhagama
akieleza sheria mbalimbali za mchezo huo kabla ya kuanza rasmi mbio
hizo.
Asa
Mwaipopo ,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ulio chini ya Kampuni ya
Acacia ,akizungumza kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yanayofanyika
kwa mwaka wa tatu katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.Wengine kutoka
kulia ni
Meneja
Uendelevu wa Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa Buzwagi,George Mkanza,Mgeni
rasmi katika mashindano hayo Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Anastazia Wambura na katikati ni Katibu wa Baraza la Michezo
(BMT) .Said Kiganja.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura
akivishwa kofia ngumu kabla ya kufungua Mashindano ya Mbio za Baiskeli
ya Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016.
Naibu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura
akiendesha baiskeli kuashiria kufunguliwa rasmi kwa mashindaano ya
Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016.
Naibu
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa
ameshika bendera ,tayari kuanzisha mbio hizo,kulia ni Meneja Mkuu wa
Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakianza mbio hizo.
Baadhi
ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Kahama na Vitongoji
vyake wakiwa barabarani kushuhudia mbio za Baiskeli za Acacia
Tufanikiwe Paomja Cycle 2016.
Mmoja wa waendesha Baiskeli akipewa maji na mmoja wa makamisaa wa mchezo huo Aman Vicent wakati mashindano hayo yakiendelea.
Meneja
wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya Madini
ya Acacia,Necta P Foya akishiriki mashindano hayo kwa upande wa wanawake
.
Umati
mkubwa wa wananchi wakiwa barabarani wakingojea kumshuhudia mshindi wa
mbio za baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Chalange 2016.
Muonekano wa picha ya juu eneo la Phantom eneo ambako mashindano hayo yalianzia na kumalizikia.
Washiriki wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 wakihitimisha mbio hizo.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog aliyeko Kahama,Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment