WAZIRI Mkuu wa zamani
wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewatembelea
wananchi wa mji wa Bukoba walioathirika na tetemeko la ardhi na kuwasihi
Watanzania kuwasaidia wananchi hao kama ilivyo desturi yetu.
Akizungumza na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu Septemba 10, 2016 alipofika
Ofisini kwake kumpa pole kufuatia tetemeko hilo lililotokea Septemba 10, 2016
na kuua watu 17. Lowassa alisema, amefika mkoani humo ili kutoa mkono wa pole
kufuatia maafa hayo na kumpapole Mkuu wa mkoa huo kwa niaba yawananchi wa mkoa
wa Kagera.
“Nawasihi watanzania wenzangu tuendelee
kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa kitaifa tulionao”.
Ameandika Lowassa katika ukurasa wake wa Tweeter.
Baada ya kuona hali
ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza ndugu zao, nyumba na mali
zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake wa Twitter kufikisha ujumbe kwa
jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo duniani kote.
Ujumbe wa kwanza
Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na mlioathirika na tetemeko,
Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki kigumu pamoja”
Lowassa akizungumza na wakazi wa Hamugembe, baada ya kutembelea eneo hio lililoathirika sana na tetemeko hilo
0 comments:
Post a Comment