2


SI LA KULIKOSA

Monday, September 26, 2016

 MWANDISHI wa habari marehemu Adolph Simon Kivamwo,aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 48, amezikwa Septemba 25, 2016 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mamia ya wanahabari, Wafanyabiashara mashuhuri, viongozi wa kisiasa, wananchi wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, walifurika kwenye mazishi hayo yaliyotanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marahemu iliyofanyika viwanja vya wazi, Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Marehemu alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya Saratani ya Utumbo na ameacha mkecna watoto wanne. Miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, Mbunge wa Chalinze, Riziwani Kikwete, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, na Mbunge wa Afrika Mashariki,  Shy-Rose Bhanji. Pia wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini walishiriki mazishi hayo


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu