Friday, September 23, 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI APANDA MABASI YA MWENDO KASI, JIJINI DAR ES SALAAM


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata tiketi ya mabasi
ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kusafiri na mabasi hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Kushoto ni Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga naye akiwa
mmoja wa wasafiri wa mabasi hayo. Masauni aliyapanda basi la Mwendo kasi mara baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu
pamoja na usalama wa abiria. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiigusisha tiketi yake
katika mashine ya Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo
jijini Dar es Salaam ili mruhusu kuingia ndani ya stendi hiyo kwa ajili ya kusafiri na mabasi
hayo kutoka katika kituo hicho kuelekea Posta. Mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiingia ndani ya Basi la
Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT katika Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kusafiri na basi hilo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa ndani ya moja ya
mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha
Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya
Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitelemka katika moja
ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam katika kituo cha
Nyerere, Posta. Masauni alipanda basi hilo akitokea Ubungo baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama
wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiondoka katika Kituo
cha Mabasi ya Mwendokasi cha Nyerere, Posta, mara baada ya kusafiri na usafiri huo akitokea
Ubungo, jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi
Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Katikati ni Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi
****************************
  • STORY STORY
    Masauni apanda mabasi ya Mwendo Kasi jijini Dar es Salaam
    Felix Mwagara, MOHA
    NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameupongeza Mradi
    wa Mabasi ya Mwendo Kasi ya UDA-RT wa jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi
    waendelee kuyatumia mabasi hayo wanaposafiri sehemu mbalimbali jijini humo.
    Mhandisi Masauni ameyasema hayo jana mara baada ya kusafiri na mabasi hayo kutoka kituo
    cha mabasi hayo cha Ubungo mpaka katikati ya jiji kwa lengo la kujionea jinsi mabasi hayo ya
    mwendokasi yanavyohudumia abiria pamoja na kuwapa moyo wananchi kuwa usafiri huo
    unatumiwa na mwananchi wa aina yeyote.
    Akizungumzia usafiri huo, Masauni alisema mradi huo umerahisisha sana usafiri kwani
    ametumia dakika chake akitokea Ubungo hadi Posta katikati ya jiji bila usumbufu wowote, hivyo
    mradi huo ameomba uendelee kulindwa pamoja na kutunzwa na UDA-RT na wananchi wenyewe
    kwa ujumla.
    “Mimi kwa kweli nimeufurahia sana usafiri huu, Serikali imefanya jambo kubwa sana kwa
    wananchi wake, kwa kuwajali wananchi kwa kuuleta mradi huu ambao unarahisisha safari kwa
    uharaka zaidi na pia unapendezesha jiji kwa jinsi magari yalivyo nadhifu,” alisema Masauni
    ambaye pia alilipa nauli kwa kupanga foleni kama wananchi wengine wanavyofanya wanapotaka
    kusafiri na usafiri huo
    .
    • Masauni aliongeza kuwa; “Nimefarijika sana na lugha ya adabu na tulivu ambayo wanaitu
      madereva wa mabasi hayo wanapowatangazia wananchi vituo mbalimbali vya kushuka na
      kuingia kwenye mabasi hayo, hii inasaidia kuwa na mawasiliano mazuri na abiria, pia inaonesha
      madereva hao wamefunzwa vizuri na wanaipenda kazi yao.”
      Hata hivyo, Masauni alitoa ushauri kwa uongozi wa mabasi hayo, kuruhusu wananchi waingie
      ndani ya mabasi hayo kwa idadi ambayo haitaleta kero kwa abiria wengine ili kupunguza wingi
      wa abiria hao kwa lengo la kuepuka mbanano mkubwa wa abiria.
      Pia aliwataka wananchi wa jiji hilo kuyatunza mabasi hayo, na pia kukubali maelekezo ya
      madereva wanapotoa matangazo wanapokuwa safarini kuelekea maeneo mbalimbali ya jiji.
      Naibu Waziri huyo alipanda mabasi hayo akitokea Ubungo mara baada ya kumaliza ziara yake
      ya kushtukiza kwa kutembelea Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kwa lengo la kukagua mabasi
      mabovu pamoja na usalama wa abiria wanaosafiri na mabasi hayo. Masauni pia alifanya ziara
      hiyo ya ghafla kwa kutembelea Stendi ya Kibaha, mkoani Pwani.
      wa idadi ambayo haitaleta kero kwa abiria wengine ili kupunguza wingi

DKT.MAGUFULI AMTEUA KAIMU OFISA MTENDAJI MKUU TTCL MPYA. Waziri Kindamba. About Richard Mwaikenda

Today Deal $50 Off : https://goo.gl/efW8Ef
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu