Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
Tanzania, Lanfang Liao (kushoto) akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa
mashindano ya sauti, Hilda Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye
ukubwa wa inchi 40 kutoka kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmojawapo wa washindi wa sindano la
vipaji vya sauti, Hilda Malecela akikumbatiana na majaji baada ya
shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio hilo kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao na kulia ni majaji na washindi
wengine. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia
fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China.
washindi 10 wa shindano la vipaji vya
sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China
Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi
hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda
kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini
Beijing, China.
Washindi 10 wa shindano la vipaji vya
sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China
Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada ya kutangazwa washindi. Washindi
hao 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda
kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini
Beijing, China.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes
Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara
baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na
StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania. Washindi 10
walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya
kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing,
China.
Mmoja wa washiriki wa shindano la
vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha uwezo wake wa kuigiza sauti
mbele ya majaji jukwaani. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo
na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya
StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja wa washiriki wa shindano la
vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya
kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Mshiriki wa shindano la vipaji vya
sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha
uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10 walipatikana katika shindano.
Na Dotto Mwaibale
Hatimaye shindano la kusaka vipaji vya
sauti lililoandaliwa na kampuni ya StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi
wa Chini nchini Tanzania limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa
watanzania 10 kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu
yake yaliyopo jijini Beijing.
Akizungumza baada ya shindano hilo Dar
es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam ambaye ndiye
aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa majaji alisema kuwa
anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila kipaji alichonacho
kwani haikuwa kazi rahisi.
‘’Kwanza kabisa nashukuru kwa ushindi
huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani ulikuwa ni mkubwa ukizingatia
washiriki walioingia hatua ya fainali wote walikuwa wana uwezo mkubwa
sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo tangu awali na hatimaye
kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza kukitoa kwa watanzania
kupitia kipaji change cha sauti. Fursa niliyoipata mimi pamoja na
washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia na kuitumia ipasavyo.’’
alisema . Malecela
‘’Napenda kuwaahidi watanzania kuwa
nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha nafanya kazi nzuri ili wao
waendelea kuburudika na kujifunza zaidi kupitia filamu na tamthiliya.
Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua umuhimu wa Kiswahili na kuja
ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini. Mara nyingi tumekuwa tukiona
mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza lakini si kwa upande wa sauti.
Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli ambayo inastahili kuigwa na
makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo aliyeongoza kwa kuwa na
alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji
Naye kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu
wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona
shindano la kusaka vipaji vya sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na
watanzania sehemu mbalimbali za nchi.
‘’Hatukutegemea kama watanzania wengi
wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni kinyume chake kwani
imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye vipaji vya sauti. Sanaa
ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii mwenyewe anavyoamua anakitumia
vipi kipaji alichonacho. StarTimes tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa
filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya
Kiswahili zinapendwa sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili
tufanye nao kazi hiyo kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema Liao
‘’Tunaamini kupitia shindano hili
tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10 watakaokwenda kujumuika na
wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing, China katika kuzalisha kazi
zilizo bora kabisa. Nawasihi washindi waliopata fursa hii kuitumia vema
kwa kufanya kazi kwa bidii kwani ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa
na majaji kuwa vinara dhidi ya wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali.
StarTimes tunaahidi kuendelea na zoezi hili wakati ujao kwani bado
uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote tupo kwa ajili ya kuwapatia kile
wateja wetu wanachokitaka.’’ alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa
StarTime nchini
Katika fainali hizo washindi wa kwanza,
pili na watatu; Hilda Malecela - kutoka DSM, Safiya Ahmed kutoka
Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka Zanzibar) walizadiwa runinga za
kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na 24 kila mmoja na StarTimes
kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika fainali hizo huku washindi
saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa kutoka StarTimes.
Kwa ujumla washindi kumi waliopatikana
ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Sadiq Kututwa(ZNZ),
Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ),
Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao(DSM), Jamila
Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM). Na wote watapata fursa ya kwenda
kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing,
China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.
Katika mashindano hayo takribani
washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika usaili uliofanyika katika
mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar (Septemba 3) na Dar es Salaam
(Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu wakabakia na kutinga hatua ya
fainali.
Washiriki 18 waliotinga hatua ya fainali
ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni Mathew Philip Mgeni, Dorcas
Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na Hilda Kinabo; Zanzibar ni
Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh, Rukia Hamdan, Imatu Obeid
Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es Salaam ni Hilda Malecela,
Abraham Richard, Happiness Stanslaus ‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel
Landey, Coletha Raymond, Jamila Hassan na Maisala Abdul.
0 comments:
Post a Comment