Thursday, September 22, 2016

Waziri Nape apokea Milioni Kumi kutoka Skol Contractors Building Limited Kusaidia Waathirika wa Tetemeko Kagera.

(a) & (b):Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kulia) kiasi cha Shilingi Milioni Kumi taslimu leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera waliyoathirika na tetemeko la ardhi liliotokea hivi karibuni.

Na Shamimu Nyaki – WHUSM
Dar es Salaam.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea  kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kutoka  Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited.

Akipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kampuni hiyo Bw. Vincent Peter Masawe  Waziri  Nnauye amemthibitishia kuwa pesa hizo zitawasilishwa  kwa waathirika wa tetemeko hilo ili zitatue changamoto zinazowakabili.

“Ninashukuru sana kwa msaada wenu mmetambua changamoto wanazopata wenzetu,niwaombe Watanzania wote tuendelee kujitoa kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa haya”.Alisema Mhe.Nnauye.
Aidha Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw.Vincent Peter Masawe amesema Kampuni yao imeguswa na matatizo waliyopata wakazi  hao wa Kagera na ndio maana  wameamua kuwasaidia ili hali zao za maisha zireje kama zamani.

“Tumeamua kuwasaidia wenzetu na tunaomba wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla popote walipo waguswe na jambo hili na waunge mkono Serikali katika juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hili”. Aliongeza Bw.Masawe.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amewakaribisha wananchi wote katika harambee ya kuchangia waathirika hao iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) itakayofanyika Septemba 21 mwaka huu jioni katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam.


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu