Meneja wa Shirika la Posta mkoani
Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta
Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's
Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Siku ya Posta duniani huadhimishwa
ifikapo Oktoba 09 kila Mwaka ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Siku ya
kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Duniani ulioanzishwa mwaka 1874 katika mji
wa Berne nchini Switzerland ukijumuisha mataifa 192 duniani.
Na BMG
Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba
na zoezi la kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Uandishi wa barua Kitaifa
kutoka mkoani Mwanza ambapo washindi watano kati ya 10 bora kitaifa
wametoka Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Washindi hao na nambari walizoshika
kwenye mabano ni, Denis Bahati Stephen (01), Samwel Lufungulo Somelo
(02), Vitalis Aloo Awasi (03), Kizito Eliakimu Paschal (04) na Fredrick
Elias Mayunga (08).
Washindi wa Tano na Sita wametoka
Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa Saba ametoka Shule ya
Lugalo mkoani Iringa, huku Washindi wa Tisa na 10 pia wakitoka Shule ya
Mazinde Juu mkoani Tanga.
Meneja wa Posta mkoani Mwanza, Julius
Chifungo amesema shindano la uandishi wa barua huwashirikisha wanafunzi
wa shule za msingi na sekondari wasiozidi umri wa miaka 15 ambapo shule
za msingi lugha ya kiswahili na kiingereza hutumika na kiingereza pekee
kwa shule za sekondari.
Amebainisha kwamba wanafunzi huandika
barua yenye mane kati ya 500 na 1,000 kulingana na mada iliyotolewa na
kwamba mwaka huu mada ilikuwa ni "Jiandikie barua ukiwa na miaka 45"
ambapo barua ya mshindi wa kwanza itakwenda kushindanishwa na barua za
washindi wengine kutoka nchi 191 wanachama wa Umoja wa Posta Duniani
ambapo mshindi wa kwanza nchini ataliwakilisha taifa kwenye shindalo
hilo nchini Switzerland.
Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo
Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye
maadhimisho hayo akizungumza ambapo amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii
katika masomo yao hususani kuwa bora kwenye kusoma, kuandika na
kuzungumza lugha nyingi tofauti na kiswahili na kiingereza.
Wanafunzi
wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu
la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho
Siku ya Posta yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
Mkuu wa Shule ya Saint Mary's (Nyegezi
Sekondari) Jijini Mwanza, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya
Posta Duniani. Siku ya Posta duniani hufanyika kila mwaka Oktoba 08,
hivyo yamefanyika leo Oktoba 07 kutokana na ratiba ilivyopangwa.
Mshindi wa Nane Kitaifa kwenye
Mashindano ya Uandishi wa barua, Fredrick Elias Mayunga kutoka Saint
Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi wa Nane amepokea Cheti cha
utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari,
Kikokoteo pamoja na fedha Elfu Arobaini (40,000).
Mshindi wa Nne Kitaifa kwenye Mashindano
ya Uandishi wa barua, Kizito Eliakimu Paschal, kutoka Saint Mary's
Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi wa Nne amepokea Cheti cha
utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari,
Kikokoteo pamoja na fedha Laki Moja na Elfu Ishirini (120,000).
Mshindi wa tatu Kitaifa kwenye
Mashindano ya Uandishi wa barua, Vitalis Aloo Awasi, kutoka Saint Mary's
Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi wa Tatu amepokea Cheti cha
utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari,
Kikokoteo pamoja na fedha Laki Mbili (200,000)
Mshindi wa Pili Kitaifa kwenye
Mashindano ya Uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint
Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi wa Pili amepokea Cheti cha
utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari,
Kikokoteo pamoja na fedha Laki Tatu (300,000)
Mshindi wa Kwanza Kitaifa kwenye
Mashindano ya Uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint
Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.
Mshindi wa kwanza amepokea Cheti cha
utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari,
Kikokoteo pamoja na fedha Laki Nne (400,000)
Mkuu wa Shule ya Saint Mary's Seminary,
Maximillian Buluma, akipokea zawadi ya shule hiyo baada ya kuwa shule
iliyotoa washindi kitaifa pamoja na washiriki wengi. Amepokea mpira
pamoja na Cheti kutoka Shirika la Posta.
Kulia ni Meneja wa Posta Mwanza, Julius Chifungo, akimkabidhi mgeni rasmi zawadi
Washindi wa shindano la kuandika barua
nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta
Mwanza, Waalimu wa Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi
pamoja na Wazazi.
Washindi wa shindano
la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini
Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazazi wao.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza.
Washindi wa shindano
la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa
shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na
Meneja wa Posta Mwanza.
Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza.
Washindi wa tatu bora katika shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza
Afisa Masoko, Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Mponda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwalimu Victor
Mgisha anayefundisha somo la Kiingereza shule ya Saint Mary's Seminary
Jijini Mwanza akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
Waalimu wa Shule
ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakielezea furaha yao baada ya
wanafunzi wa shule hiyo kuibuka washindi wa shindano la uandishi wa
barua linaloandaliwa na Umoja wa Posta duniani na kufanyika kwa nchi
wanachama 191 kote duniani.
Mwalimu wa Shule ya
Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, akisoma barua iliyompa ushindi,
mshindi wa kwanza kwenye shindano la uandishi wa barua nchini.
Meneja wa Shirika la
Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya
Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya
Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
Mshindi wa kwanza
Kitaifa kwenye shindano ya uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen,
kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika
leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini
Mwanza.
Mshindi wa pili Kitaifa katika shindano ya uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza
kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika
leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini
Mwanza.
Bonyeza HAPA Kutazama Mwanza walivyoibuka kidedea kwenye Shindano la Uandishi wa barua mwaka 2015 Kitaifa
0 comments:
Post a Comment