Tuesday, October 11, 2016


  Naibu Waziri, akiangalia kiatu kilichotengenezwa kwenye kiwanda cha viatu Karanga, kilichko gereza kuu la Karanga mjini Moshim, mkao wa Kilimanjaro, wakati wa ziara yake ya kikazi majuzi, ambapo pia alitembelea mpaka wa Tanzania na Kenya, wa Tarakea ulioko wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro
 Naibu Waziri, akiangalia kiatu kilichotengenezwa kwenye kiwanda hicho

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ya utengenezaji wa viatu kiwandani hapo.

 Naibu Waziriakiwasili eneola mpakani


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimajaro alipotembela mpaka wa Tarakea wilayani Rombo Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun akipewa maelezo na Afisa Mipaka Holili Michel Amo, juu ya jiwe  linaloonyesha mpaka wa Tanzania na Kenya lililopo katika mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na watu wasiojulikana hivyo kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja na wafanyabiashara za magendo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun akionyeshwa Mpaka katika picha unaotenganisha Tanzania na Kenya ulioko Holili wilayani Rombo alipofanya zaiara ya siku moja ya kikazi kuangalia mipaka hiyo na kutoa maelekezo kwa wahusika wa kulinda mipaka hiyo namna ya kuweza kukabilina na changamoto zilizopo katika mpaka huo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni  akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Karanga, Kamishna Msaaidizi wa Magereza, (ACP), Mkwiche  mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara katikaa Kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo ili kujionea  uzalishaji wa bidhaa za viatu ambavyo Rais Magufuli alitaka majeshi yote nchini kutumia viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akipokewa na maafisa wa Gereza la Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha kutengeneza viatu kinachomilikiwa na jeshi hilo


NA MWANDISHI MAALUM, MOSHI
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni avitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kuzidi kuimarisha ulinzi katika mipaka ili kushirikiana na Serikali katika mpango wa kupambana na uhalifu  nchini.
Masauni aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara katika mipaka ya Tarakea  na Holili iliyopo mkoani Kilimanjaro ili kujione changamoto zinazojitokeza katika mipaka hiyo ambapo tarifa zinaonyesha kwamba kuna njia zisizo rasmi zaidi ya 265 zinazotumiwa kuptisha bidhaa za magendo na wahamiaji haramu
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Masauni alivitaka vyombo vyote vya ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha vinaashirikiana kila mtu kwa nafasi yake ili kupambana na uhalifu wa kupitisha bidhaa za magendo zinazopitishwa katika mipaka hiyo na kuikosehsa serikali mapato.
Masauni alisema kuwa Serikali ya awamu ya Tano ina dhamira ya kupeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo ni lazima kwa vyombo hivyo kudhibiti biashara zote zinazopita kimagendo mipakani humo lakini pia kuepuka rushwa ili kupiga hatua mbele za kimaendeleo.
Pamoja na kuwapo kwa changamoto ya nguvu kazi na vitendea kazi serikali itahakikisha inaaandaa maofisa wa kutosha mipakani humo ili kuongeza nguvu kazi wakati wa operesheni zao na doria wakati wote.
Aidha Masauni ametoa rai kwa watumishi wa vyombo hivyo kujiepusha na tabia ya kushirikiana au kuwaficha wafanyabiaashara wanao jihusishaa na biashara ya maagendo.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwqaandanizi Wilbrod Muutafungwa almueleza naibu Waziri huyo licha ya changamoto zilizopo wanaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka kwa kufanya doria mara kwa mara licha ya kwamba wafanyabiashara hao wa bidhaa za magendo kutumia mbinu mbalimbali kukwepa ushuru lakini Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeweza kuwatia mbaroni.
Awali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun aliliagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi na nje.
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii akilini maofisa wa majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.
Masauni alisema kwamba dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo Jeshi la Magerezaa kupitia kiwanda chake na miradi mingine mingi halina budi kuendelea kuzidisha kuzalisha viatu bora vitakavyo kidhi kiwango cha uhitaji na soko ili kukuza uchumi wao na Serikali kwa ujumla.
Aidha, katika ziara yake, Naibu Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu Jeshi hilo kufanya miradi mingi kwa ustadi mkubwa ili kujipatia psa zitakazosaidia kujiendesha wao kama jeshi na mashirika mengine yanayounga mkono miradi yao hivyo kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri huyo alilipongeza Jeshi hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulinganisha na nyingine zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi kutengeneza viatu bora zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani na nje ya nchi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu