Friday, October 28, 2016

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, (Kushoto), akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi  Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini  makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, Oktoba 27, 2016
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia  €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu