Sunday, October 16, 2016

WANAUME WA KATOLIKI JIMBO LA DAR ES SALAAM WATEMBELEA MASISTA WA DADA WADOGO WA MTAKATIFU FRANSISKO MBAGALA
 Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa  Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu  wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakinunua mvinyo wa Arovela.
Waumini wakisali mbele ya msalaba nje ya kibanda maalumu cha msalaba wa Yesu.
waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
waumini wakitafakari katika ibada hiyo.
Makofi yakipigwa wakati maandamano yakiingia kabla ya kuanza kwa ibada hiyo.
Picha zikipigwa katika ibada hiyo.
Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Kanisa Katoliki Mbagala Kizuiani wakiimba katika ibada hiyo.

Ma padri mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo.
Masista wa shirika hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika ibada hiyo.


Kiongozi wa kwaya hiyo, Fednandi Constantino akifanya vitu vyake.
Ibada ikiendelea.



Monsinyori Mbiku   akiongoza ibada hiyo.
Waumini wakipokea sakramenti ya Ekaristi Takatifu.
Kinanda kikipigwa.
waumini wakipiga picha za matukio mbalimbali.
Mapadri na watumishi wa kanisa wakitoka kwenye ibada hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.

Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika  la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.

“Tusidharau tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.


Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.

“Nyerere aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin. Tanzania haikuzoea vita.
“Hivyo aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda. 

Nyerere  alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisemaMbiku.

Vita kati ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979 baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).

Kutokana na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka  kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na kanisa.

“Masista  wanajitoleakuombea kanisa na watu wote  wapate wokovu pasipo kubagua dini zao. Sala yao  nimuhimu, ina nguvu na Mungu anaisikiliza kwa kujitoa kwao,” alisema.
Kwa msingi  huoaliwaomba Uwaka ambao kaulimbiu  yao “Nguzo Imara Hekalu la Bwana” 


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu