Na Jacquiline Mrisho – Dodoma.
Jumla
ya askari 152 wamefukuzwa kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu ya
kukiuka Sheria, Taratibu na Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa katika
Kanuni za Kudumu za Polisi (PGO) namba 103.
Idadi
ya askari hao waliofukuzwa kazi imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Maryam Msabaha aliyehitaji kufahamu juu ya idadi ya
askari waliochukuliwa hatua kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Mhandisi
Masauni amesema kuwa kazi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda raia, mali
zao pamoja na mipaka ya nchi lakini kuna baadhi ya askari hao wanakwenda
kinyume na Sheria kwa kuwapiga wananchi na kuwasababishia ulemavu pamoja na
vifo hivyo Jeshi hilo limewachukulia hatua za kinidhamu.
“Jeshi
la Polisi hufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo lakini
kuna baadhi ya askari wamekuwa wakikiuka maadili na mwenendo mwema wa Jeshi
letu hivyo kuanzia Januari 2015 hadi Juni 2016 tuliwachukulia hatua za
kinidhamu askari 200”, alisema Mhandisi Masauni.
Naibu
Waziri huyo amefafanua kuwa baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu,
walifanyiwa uchunguzi wa kina na jumla ya askari 152 kati ya 200 walikutwa na
hatia hivyo hatua iliyofata ni kuwafukuza kazi.
Akizungumzia
kuhusu mpango wa Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi, Mhandisi
Masauni amesema kuwa wanatambua tatizo la makazi ya Askari Polisi katika maeneo
mbalimbali nchini hususani kwenye mikoa mipya hivyo Serikali ina nia ya kutatua
tatizo hilo kwa kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya askari hao.
“Serikali
imedhamiria kupunguza tatizo la upu
ngufu wa makazi ya askari polisi kwa kujenga
nyumba kwa awamu kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba 4,136 nchi nzima ambao
utaanza kutekelezwa baada ya taratibu za mkopo wa kuwezesha ujenzi huu
kukamilika”, aliongeza Mhandisi Masauni.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment