Diwani
wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala Mtimika
(Kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa Bank ya Amana nchini Dr Mosen Masoud
wakikata utepe Kuashiria kuzinduliwa Rasmi kwa Huduma ya mikopo Midogo
Midogo kwa wafanya biashara wa Mbagala Jijini Dar es salaam.uzinduzi huo
umefanyika katika Tawi la Amana Mbagala(Picha zote na Vicent Macha wa Habari24 blog)
|
Hatimaye
wakazi wa mbagala wanaofanya Biashara ndogo ndogo wakiwemo
wajasiriamali wamepata neema kubwa baada ya Bank ya AMANA kuzinduaa
huduma yake mpya ya kutoa mikopo midogo midogo kwa wafanya biashara,
huduma ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni miaka
mitano Tangu kuanzishwa kwa Bank Hiyo.
Akizungumza
na wanahabari na wananchi wa mbagala ambapo ndio uzinduzi huo
umefanyika Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud amesema kuwa huduma
hiyo imeanzishwa mahususi kwa kutambua hitajio kubwa katika jamii la
wafanya biashara wadogo wadogo katika kupata mtaji ya kukuza biashara
zao hivyo Bank ya Amana imeamua kuwainua wafanya biashara hao wadogo ili
kuinuka kipato chao na kufikia kipato cha kati na hata kipato cha juu.
Amesema
kuwa kupitia huduma hiyo Amana Bank inawawezesha wafanya biashara kwa
kununua bidhaa wanazohitaji katika biashara zao na kuwauzia kwa bei
nafuu kwa mkopo ambapo watarejesha kidogo kidogo katika muda ambao
umewekwa katika utaratibu.
Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud akizungumza na wanahabari na wananchi waliofika katika uzinduzi huo
|
Ameongeza
kuwa wafanyabiashara sasa wana nafasi ya kukodishwa vifaa mbalimbali
wanavyohitaji katika kuendesha biashara zao kwa kodi nafuu na mwishowe
wanaweza wakanunua vifaa hivyo kwa Bei nafuu
Mkurugenzi
huyo ameendelea kueleza kuwa kwa sasa Huduma hiyo ya mkopo imeanza
kutolewa kwa wateja wake wanaotumia Tawi lao la Mbagala tu lakini kusudi
lao ni kuhakikisha kuwa wanaendesha zoezi hiyo latika matawi yao yote
nchini ambayo kwa sasa yapo matawi saba.
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es salaam Mh Abdala Mtimika Akizungumza
|
Akizunguza
wakati wa uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya
Kibondemaji Abdala Mtimika ambaye alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Temeke
amesema kuwa Uzinduzi wa Huduma hiyo ya kutoa mikopo midogo modogo sasa
imekuja wakati muafaka kipindi ambacho watanzania wengi wamekuwa
wakilalamika kudorora kwa uchumi na pesa kupotea hivyo ni jukumu la
wafanya biashara wa mbagala kutumia nafasi hiyo adhimi kuhakikisha kuwa
wanapata mikopo hiyo na kuwekeza katika Biashara zao.
Wiki ya Huduma kwa wateja ikiendelea wateja mbalimbali wakipata Huduma katika Tawi la Benk hiyo Mbagala leo
|
Aidha
Diwani huyo amewapongeza sana uongozi wa Bank ya Amana Tanzania kwa
kuweza kuendesha Bank hiyo kwa usawa pamoja na kuwa imekuwa ikijulikana
kuwa Ni Bank ya kiislam ila sio kweli kwani imekuwa ikitoa Huduma kwa
watanzania wote bila kujali Dini zao pamoja na kuwa inatumia Taratibu za
kiislam.
Wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
|
Uzinduzi
wa huduma hiyo umekwenda sambamba na uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa
mteja ambapo bank hiyo imeanza kuadhimisha wiki hiyo leo ikiwa ni
kuendelea kusherekea miaka Mitano ya Bank hiyo tangu ianze kutoa huduma
za kibenk nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment