Wednesday, November 9, 2016



NA K-VIS MEDIA/MASHIRIKA YA HABARI
WAMAREKANI wameamua tajiri mkubwa Donald Trump kutoka chama cha Republican kuwa Rais wa 45 wa nchi hiyo, baada ya matokeo ya kura kuonyesha, ameshinda uchaguzi huo kwa kupata alama 276 dhidi ya alama 218 za mpinzani wake toka chama cha Democrat, mwanamama Hillary.
Kinyume na matarajio ya wengi kuwa Trump ambaye wakati wa kampeni alikuwa akikabiliwa na shutuma kadhaa za kibaguzi na uzalilishaji, alipewa nafasi ndogo ya kumshinda mpinzani wake, Bibi. Hillary Clinton wa chama cha Democrat.
Donald John Trump alizaliwa mwaka 1946, huko Queens, jijini New York, akiwa ni mototo wa nne wa familia ya Bw.Frederick C, na Mary MacLeod Trump.
Baba yake Bw.Frederick Trump, alikuwa mjenzi na muendelezaji wa majumba ya kibiashara, (kupangisha), akiwa amejikita zaiidi katika masuala ya ujenzi wa nyumba za watu wa kipato cha kati (Middle income apartments) huko Queens, Staten Island na sehemu Fulani huko Brooklyn, New York.
Donald Trump, alikuwa ni kijana mwenye nguvu na akili nyingi, na wazazi wake walimpeleka shule ya kijeshi huko New York akiwa na umri wa miaka 13, wakitegemea nidhamu ya shule za kijeshi zitawezesha matumizi bora ya nguvu alizokuwa nazo.
Trump alifanya vizuri shuleni katika Nyanja za kushirikiana na wenzake lakini pia kimasomo na kimfanya kuwa “nyota” na kio ngozi wa wanafunzi wakati akihitimu mwaka 1964.
Wakati wa mapumziko ya majira ya kiangazi, Trump alifanya kazi za baba yake za ujenzi, na alijiunga na chuo kikuu cha Fordham, na baadaye kuhamia shule ya masuala ya fedha ya Wharton, chuo kikuu cha Pennsylvania na kuhitimu mwaka 1968 akiwa na shahada ya uchumi.
Trump alijiunga moja kwa moja na shughuli za biashara ya baba yake, (Trump Organisation) mnamo mwaka 1971 na kufanya makazi yake pale Manhattan na akawa maarufu miongoni mwa watu maarufu.
Trump akaanza kupata tenda kubwa kubwa za ujenzi wa majengo pale Manhattan na hivyo kujiingizia mabilioni ya dola na kazi yake ilizidi kukua siku hadi siku na kumuongezea umaarufu. Donald Trump si mwanasiasa, yeye anachojua sana ni biashara, amekuwa mwanzilishi, Mwenyekiti, Rais, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Trump Organization kuanzia mwaka 1975 hadi sasa.
Pia ni Mwenyekiti wa Mahoteli   na Makasino ya Trump, Donald J. Trump amemuoa Melania na ana watoto watano, Donald Jr. Ivanka, Tiffany na Barron.
Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo, Mgombea mwenza, Pence ndiye alikuwa wa kwanza kujitokeza kwenye jukwaa akiwa na familia yake. "Wamarekani wameongea, wamemchagua mshindi, rais mpya wa Marekani, Donald Trump." alisema Pence.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi kwenye kambi yake mbele ya wafuasi lukuki mjini New York, Donald Trump akifuatana na mkewe na familia yake, alisema "Asanteni, asanteni sana, samahani kwa kusubiri sana, maana kulikuwa na mkorogo, asanteni sana, nimepokea simu kutoka kwa mama Clinton, anatupongeza na mimi ninampongeza yeye na familia yake." Alisema.
Ni taimu kwetu kuwa wamoja kama wamarekani, Nitakuwa rais wa Wamarekani wote ni hii ndiyo muhimu kwangu.   
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu