2


SI LA KULIKOSA

Friday, November 11, 2016

 Jeneza lenye mwili wa Mbunge wa Dimani, Zanzibar, marehemu Hafidh Ali Tahir, ukipandishwa kwenye ndege kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma, leo Novemba 11, 2016 kupelekwa kisiwani Unguja kwa mazishi. Marehemu Hafidh ambaye alikuwa mjini Dodoma akihudhuria vikao vya bunge, alifariki ghafla alfajiri ya leo Novemba 11, kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma alikokwenda yeye mwenyewe kupatiwa matibabu baada ya kujsikia vibaya. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, aliwaongoza wabunge kuuaga mwili wa marehemu kwenye jengo la bunge mjini Dodoma. Taarifa kutoka Zanzibar zinasema, tayari mwili wa marehemu umewasili kisiwani Zanzibar na mazishi yatafanyika baada ya sala ya Alasiri leo hii

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani,   Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia  mjijini Dodoma usiku wa kuamkia leo. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (wapili kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama  (wakwanza kushoto) na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe (wakwanza kulia) na wabunge wengine  wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma tayari kutoa heshima za mwisho
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha zake

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu