Na
Theresia Mwami TEMESA Songea
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu, leo ametembelea
na kukagua karakana ya TEMESA iliyopo Songea Mkoani Ruvuma na kumuagiza Meneja
wake, Mhandisi Elisha Mulyila kuhakikisha Mashine zote zilizomo kwenye karakana
ya vyuma zinafanyiwa ukarabati.
Dkt
Mgwatu ameongeza kuwa ukarabati wa mashine hizo uzingatie ubora na utumie
wataalamu wa ndani ya nchi ili kuwajenge uwezo wataalamu hao katika
utengenezaji na ukarabati wa mashine mbalimbali.
Pia
Dkt. Mgwatu alimuagiza Meneja huyo
kuhakikisha kuwa kituo kinaibua kazi mbali mbali za utengenezaji vipuri kwa
kutumia karakana ya uchongaji vyuma iliyopo kituoni hapo, kwani karakana hiyo inauwezo mkubwa wa kuweza kutosheleza mahitaji
ya soko la uchongaji vyuma mkoani humo.
Kwa
upande wake Meneja wa TEMESA Songea Mhandisi Elisha Mulyila alimuakikishia
Mtendaji Mkuu huyo kuwa agizo lake litafanyiwa kazi kwa kuanza ukarabati wa
mashine na vitendea kazi mara moja ili kuendelea na majukumu yao ya kila siku
ya kuhudima vifaa muhimu hasa magari ya Serikali na Taasisi nyingine.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu
yupo katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo nyanda za juu
Kusini ili kubaini changamoto mbali mbali zilizo kwenye vituo hivyo na
kuzitafutia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment