Tuesday, November 22, 2016

TANESCO KIGOMA YADAIWA MILLIONI 41 NA TEMESA

Na Theresia Mwami TEMESA Kigoma

Shirika la umeme Tanzania TANESCO linadaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kigoma kiasi cha shilingi milioni 41 ikiwa ni malimbikizo ya madeni kutokana na matengenezo ya magari mbalimbali yaliyofanywa na shirika hilo mkoani humo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kigoma Mhandisi Hassan Karonda alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu alipotembelea kituoni hapo.

Meneja huyo ameeleza kuwa kwa sasa TEMESA Kigoma ipo kaytika operesheni ya kukusanya madeni kutoka kwa Taasisi na makampuni wanayoyadai.

“Mtendaji  Mkuu tunazidai Taasisi mablimbali kiwemo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO shilling million 41 mpaka sasa” alisema Mhandisi Karonda.

Hata hivyo Dkt. Mgwatu alimtaka Mhandisi Karonda kuhakikisha kuwa anakusanya madeni yote anayodai  mkoani humo haraka iwezekanavyo.

 “ Fuatilia ofisi kwa ofisi kukusanya madeni ili kukiwezesha kituo hiki kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa” alisisitiza Dkt. Mgwatu.

Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo Dkt. Mgwatu pia alipata fursa ya kutembelea  kivuko cha MV. Malagarasi na kuona utendaji kazi wake.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA nchi nzima kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo. 
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu