Wednesday, November 2, 2016

TEMESA LINDI



Na Theresia Mwami TEMESA Lindi

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amepongeza utaratibu unaotumika katika kituo cha TEMESA Lindi na karakana zake kwa kuratibu vizuri kazi za kila siku.

“Nawapongeza sana kwa utendaji wenu wa kazi kwa kuweka utaratibu wa kufuatilia kila kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kituo” alisema  Dkt. Mgwatu.

Dkt Mgwatu amemuagiza  Meneja wa TEMESA Mkoa wa Lindi Mhandisi Greyson Maleko kuhakikisha kuwa magari yote ya Serikali mkoani Lindi yanafanyiwa matengenezo katika karakana ya TEMESA iliyopo mkoani humo.

Dkt. Mgwatu amemtaka Meneja huyo kuhakikisha anakusanya madeni yote wanayodai kwenye Taasisi, Halmashauri na I
dara mbalimbali za Serikali kutokana na matengenezo ya magari na mitambo, sambamba na kulipa madeni yote wanayodaiwa na wazabuni kwa kipindi cha Julai-Septemba, 2016.

Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Lindi alisema kuwa changamoto kubwa inayokabili kituo hicho ni uwepo wa madeni makubwa wanayodai kwenye Taasisi na Halmashauri mbali mbali za serikali zilizopo Mkoani Lindi kutokana na matengenezo ya magari na mitambo lakini wanajitaidi kuendelea kufanya kazi kwa ustadi na kujituma.

Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu alitembelea eneo litakalojengwa gati kwa ajili ya kivuko kutoka Lindi hadi Kitunda.
Dkt. Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara ili kujionea hali ya Vituo katika mikoa hiyo pamoja na utendaji kazi wake.

MWISHO.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu