Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli, akizungumza na waandishi wa habari akiwa na
Mmiliki wa Kampuni ya kuzalisha saruji, DANGOTE kilichoko Mtwara, Alhaji
Aliko Dangote, (katikati) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles
Mwijage, baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam, Desemba 10,
2016.
NA K-VIS MEDIA
MMILIKI wa kiwanda cha kuzalisha saruji
DANGOTE kilichoko Mtwara, Alhaji Aliko Dangote, amevilaumu vyombo vya
habari kwa uzushi kuwa anataka kufunga kiwanda chake na badala yake
amesema, atawekeza zaidi hapa nchini na kwa kuhakikisha utayari wake,
ameagiza malori 600 ya kusambaza saruji na tayari batch ya kwanza ya
malori hayoyamewasili bandarini.
"Kazi yetu hapa Tanzania ni kuja
kuzalisha ajira hapa nchini, DANGOTE haina mpango wa kuingiza malighafi
ya kuzalisha saruji au nishati kutoka nje, wakati vitu vyote hivyo
vinapatikana hapa nchini." Alisema Dangote katika mazungumzo na
waandishi wa habari ambapo Rais Magufuli alikuwepo.
Alhaji Dangote amemuhakikishia Rais
Magufuli kuwa, uzalishaji wa saruji utaanza tena hivi karibuni baada ya
marekebisho fulani yaliyokuwa yakifanywa kiwandani kukamilika.
"Kama ni kweli ningekuwa nimetofautiana
na serikali, nisingeweza kuagiza malori haya mapya kuja hapa nchini, na
Rais nimemuhakikishia kuwa DANGOTE haikubaliani na kuingiza malighafi
za kuzalisha saruji na badala yake tutasaidia viwanda hivyo vya
kuzalisha malighafi ili kufikia lengo, kuingiza malighafi zinazopatikana
hapa ni kuingiza umasikini na hilo halitawezekana, na nitaendelea
kuwekeza hapa Tanzania, tumeshawekeza Dola milioni 600 kwenye kiwanda
cha saruji na tutawekeza zaidi kwenye eneo la kilimo, asante sana Mhe.
Rais." Alitoa hakikisho Mfanyabiashara huyo tajiri zaidi barani Afrika.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amesema wataifuta
kampuni ya Aqua baada ya kusababisha mtafaruku baina ya kiwanda cha
DANGOTE, serikali na wananchi kwa kutaka "kupiga dili".
"Tatizo la watanzania ni watu hawa wa
katikati, hapakuwa na taizo lakini pamekuwepo na watu wapiga dili kwenye
mradi huu, badala ya DANGOTE kununua gesi moja kwa moja TPDC ambacho ni
chombo cha serikali anaingia mtu katikati pale ili atengeneze
kamisheni, tunataka eneo kwa ajili ya JET, kaeneo kadogo tu watu
wanataka zilipwe bilioni 43 kanakwamba watu wanachukua maeneo kule
kusudi wakalipwe compensation, (fidia), kwahiyo wapiga dili ndio
walikuwa wameingilia huu mradi kwahiyo wameshindwa na walegee." Alisema
Rais Magufuli.
Rais pia alisema, " Walijiingiza
wanasiasa, matapeli sijui na wanani, na wale sisi serikali tuta deal
nao, kuna likampuni limejiingiza hapa katikati sijui linaitwa aqua,
sijui nini, hili linafutiliwa mbali." Alisema Rais Magufuli. Kwa habari
zaidi taarifa kamili ya Ikulu inapatikana hapo chini.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa
Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada
ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais akiagana na Alhaji Dangote
Mmiliki wa
Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote
akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakwanza kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe
Magufuli, akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Mmiliki wa Kampuni
ya kuzalisha saruji, DANGOTE kilichoko Mtwara, Alhaji Aliko Dangote,
(katikati) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, (kulia) na
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (wakwanza
kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Kapulya Musomba (wapili kushoto), baada ya
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam, Desemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment