George
Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto
FirePro ya Cyprus akionyesha moja ya kifaa cha kuzima moto kinachoweza
kufungwa katika mitambo mbalimbali chenye uwezo wa kuzima moto katika
hatua za awali kabisa kabla ya kuwa mkubwa wakati alipokuwa akielezea
ubora wa vifaa hivyo katika kupambana na majanga ya moto kwenye uzinduzi
ulifanyika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishono mwa
wiki.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni
inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa
akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika
mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay
jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na wa tatu ni Fikili
S. Salla Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya moto Jeshi la
Zimamoto.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni
inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa
akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika
mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay
jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni
inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa
akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika
mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay
jijini Dar es salaam , wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(kushoto), akimpongeza George Michael Mtaalam kutoka kampuni
inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus mara baada ya
kumaliza kutoa maelezo yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi
uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam,
katikati ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco
Group Campanies
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of Companies
Limited Bw. Anic Kashashaakizungimza katika uzinduzi huo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho cha Firepro mwishoni mwa
wiki.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya ,
Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
na George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya
kuzima moto FirePro ya Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa kampuni hiyo

................................................................................
Kampuni
ya JUNACO Group of Companies mwishoni mwa wiki ilizindua kifaa cha
kisasa kinachotumika kuzima moto kwenye makazi ya watu na mitambo
kinachofahamika kama ‘FirePro’ ikiwa ni uvumbuzi unaolenga kukabiliana
na janga hilo hatari.
Akizungumza
wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa kifaa hicho iliyofanyika jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhuduriwa pia na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambao ya Ndani Balozi Hassani Simba Yahya, Mwenyekiti na
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya nchini hapa nchini , Bw Justine
Lambert alisema matumizi ya kifaa hicho miongoni mwa watanzania
yatasaidia kutaondoa athari za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na
majanga ya moto kwenye makazi ya watu.
“Uvumbuzi
na ujio wa kifaa hiki ni ishara kwamba athari zitokazo na majanga ya
moto ambayo yamekuwa yakiripotiwa kupoteza maisha ya watanzania na
kusababisha umasikini kutoka na uharibifu wa mali sasa linakwenda
kwisha,’’ alisema Bw Lambert huku akiongeza kuwa wao kama sekta binafsi
wana wajibu wa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto
zinazowakabili wananchi wake.
Alisema
mbali na suala la kuhakikisha usalama wa watanzania, uwepo wa kifaa
hicho pia utaongeza ajira kwa wadau wote watakaohusika kwa namna moja au
nyingine katika mauzo ya kifaa hicho hapa nchini.
“
Ndani ya miaka minne ijayo Junaco Group of Companies tunarajia
kutengeneza ajira zipatazo 780 zitakazohusisha wauzaji, wasambazaji na
wataalamu wa kufunga kifaa hiki kote nchini,’’ alisema.
Kwa upande wake balozi Simba ambae alimuwakilisha waziri wa wizara hiyo
Bw Mwigulu Nchemba alisema serikali imekuwa ikiridhishwa sana hasa pale
inapopokea taarifa za uwepo wa teknolojia mpya zinazolenga kutatua
changamoto zinazowakibili wananchi wake kuisalama kama hiyo ya uzinduzi
wa kifaa cha ‘FirePro’ huku akitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia fursa
za kiuwekezaji kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa kama hivyo hapa
nchini.
“Ujio
wa kifaa hiki hapa nchini ni wazi kuwa utakuwa na matokeo chanya
kijamii na kiuchumi kwasababu mbali na kulinda usalama wa wananchi na
mali zao lakini pia utazalisha ajira zaidi ya 800... hongereni sana
naimani mtafikiria pia kuanzisha kiwanda kitakachowezesha uzalishaji wa
vifaa hivi hapa nchini,’’ alisema.
Kwa
mujibu wa Meneja Maendeleo wa Mradi huo Bw, George Michael, teknolijia
iliyotumika kutengeza kifaa hicho ni bora zaidi kwa nchi zinazoendelea
na ni rafiki pia kwa mazingira.
0 comments:
Post a Comment