|
Mwendesha
mifumo ya umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha kupoza
na
kusambaza umeme (Zuzu Sub-station), Bw. P.H. Rashid akitoa maelezo ya
kiufundi
kuhusu mabadiliko ya kimfumo yaliyoletwa na mradi wa Backbone wa ujenzi
wa
miundombinu ya kusafirisha umeme kuanzia mkoani Iringa hadi Shinyanga
kupitia
mikoa ya Dodoma na Singida, wakati wahariri wa vyombo vya habari
walipotembelea kituo
hicho. Kipande cha mradi huo kutoka Dodoma hadi Singida, kitawashwa leo
mkoani Singida na hivyo kuufanya mfumo huo mpya wa usafirishaji umeme
wenye urefu wa kilomita 670, kukamilika, Meneja wa mradi huo
anayeshughulikia mfumo wa usafirishaji, Mhandisi Oscar Kanyama alisema.
|
|
Wahariri
wa vyombo vya habari wakipatiwa maelezo ya kiufundi na wahandisi wa
TANESCO kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu mkoani
Dodoma ambacho kimepanuliwa chini ya mradi mkubwa wa umeme wa Backbone |
|
Meneja
Mradi mkubwa wa umeme wa Backbone, unaoendeshwa na serikali kupitia Shirika la
Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), na Kaimu Meneja
Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji kituo cha kupoza umeme cha Kibaoni mkoani
Singida wakati wa ziara ya wahariri vyombo vya habari mkoani kutembelea mradi huo
Desemba 20, 2016
|
|
Mdhibiti
wa mifumo ya umeme kituo cha kupoza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma, Bi.
Itika Alexander, akiwa kazini wakati wahariri wa vyombo vya habari
walipotembelea kituo hicho Desemba 20, 2016. |
|
|
|
|
|
Minara
mikubwa na ya kisasa ya kusafirisha umeme mkubwa (High tension),
iliyojengwa chini ya mradi wa Backbone ikionekana kandokando ya barabara
ya Dodoma-Singida |
|
Mkuu
wa kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Zuzu mkoani Dodoma,
Mhandisi, Joseph Mongi, akitoa maelezo ya kiufundi kuhusu hatua mpya
iliyopigwa na TANESCO katika kuimarisha miundombinu ya kusafirisha umeme
wa kilovolti 400 wa Backbone kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga
kupitia Dodoma na Singida. |
|
Wahariri wakipatiwa maelezo |
|
Kituo cha Zuzu cha kuposa na kusambaza umeme |
Reactors mpya zilizojengwa kwenye kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Zuzu mkoani Dodoma
|
Baadhi ya wahariri na afisa wa TANESCO kutoka kitengo cha Mahusiano, (kulia) |
|
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu ambacho kimepanuliwa chini ya mradi wa Backbone |
|
Meneja mradi wa
Baackbobe(transmission lines), Mhandisi Oscar Kanyama(mbele kulia),
akiobgoza wahariri kutembelea kituo cha Singida. |
Posted by KHALFAN SAID on 12:42
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,
Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafao ya Fidia na na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa
niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia).
.(
PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)
0 comments:
Post a Comment