Friday, December 16, 2016

TIGO YAZINDUA DUKA LA 'TEAM LEADERS' DEVIS CORNER TANDIKA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM ILI KUKUZA UJASIRIAMALI
 Msimamizi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tigo Dar es Salaam na Zanzibar, Nderingo Materu (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka dogo la Tigo Tandika Devis Corner leo.  Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Wilaya ya Temeke, Fadhila Saidi, Mwendeshaji wa duka hilo, Khadija  Matambo na kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Isack Shoo.
 Hawa ndio waendeshaji wa duka hilo. Kutoka kushoto ni Victor Juma, David Ngwale na kiongozi wao Khadija Matambo.
 Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja , Isaack Shoo akihojiwa na wanahabari.
 Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa duka hilo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya  Tigo inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tanzania,  leo imezindua rasmi mpangbo mdogo wa maduka ya huduma kwa wateja  unaofahamika  kama maduka ya Team Leaders ambayo  yatatoa huduma za kampuni  moja kwa moja kutoka maeneo wanayokaa wateja. 

Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja , Isaack Shoo maduka hayo kimsingi yatakuwepo katika maeneo ya makazi  na yatatoa huduma zote  za Tigo na miongoni mwake ni pamoja na  kurudisha  kadi za simu  zilizopotea, mauzo ya muda wa maongezi, huduma za Tigo Pesa, mauzo ya kadi za Tigo na mauzo ya simu za kisasa (Smartphones).

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari  uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Shoo alisema, “Kupitia maduka ya team leaders Tigo imejikita kuhakikisha kuwa bidhaa zakehuduma zake zimo karibu na  wateja, kuwezesha wateja wetu  kufurahia huduma  namba moja  ambayo  imo moja kwa moja  katika kujikita  kwetu  katika mabadiliko ya kuboresha mtindo wa maisha ya kidijitali.”

Shoo alisema kuwa kila  duka litakuwa na mawakala watano wa  huduma kwa mteja  ambao watakuwa wamepata mafunzo  yanayohusiana na huduma kwa mteja  kutoka Tigo  ili kukidhi mahitaji ya wateja.

Aliongeza kuwa hadi sasa maduka  yapo maduka matano  ambayo yapo Mbande, Tandika, Tabata, Segerea na  Ukonga (yote yapo Dar es Salaam) na tayari yanafanya kazi. 

Shoo aliongeza, “Maduka zaidi yanatarajiwa kuanzishwa  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  ambapo yatakuwa katika maeneo ya Kawe, Mawasiliano Towers, Kimara, Kigogo na Mwananyamala.”

Mbali na mafunzo Tigo pia itatoa  vifaa  muhimu kwa ajili ya biashara kwa mawakala wake katika hatua ya mwanzo ya kuanzisha biashara  katika maduka, jambo ambalo ni muhimu na linalothibbitisha  kujikita kwa kampuni hiyo ya simu katika  kuisaidia serikali  kstiks juhudi zake za kiupunguza  ukosefu wa ajira nchini.

Hivi sasa Tigo ina maduka maduka makubwa 50  kwa ajili ya huduma kwa wateja yaliyoasambaa  kote nchini  yakiwa na uwezo wa kuhudumia wateja kati ya 200 na 300 kwa siku.



Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu