chezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Yanga na Jamuhuri Unafanyika Usiki Huu Timu ya Yanga Imeshinda 6--0
Wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika wanaoshiriki Kombe la Mapinduzi Cup
wakiwa katika uwanja wa Amasan Zanzibar wakisubiri kukaguliwa na kuaza
mchezo wao wa kwanza na Timu ya Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan
Zanzibar Timu ya Yanga Afrika imeshenda mchezo huo kwa bao 6-0.
Kikosi cha Timu ya Jamuhri kutoka Pemba kinachoshiriki Michuano ya Kombe
la Mapinduzi Cup, kilikubali kipigo cha bao 6-0 dhidi ya Timu ya Yanga
Afrika mchezo uliofanyika usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi inashirikisha Timu Tisa kutoka
Zanzibar Uganda na Tanzania Bara.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na
wachezaji wa Timu ya Jamuhuri kabla ya kuaza kwa mchezo wao na Timu ya
Yanga Afrika uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku,
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na
waamuzi wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Timu ya Yanga na
Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Mzee Ali Haji akisalimiana na
wachezaji wa Timu ya Yanga Afrika kabla ya kuaza kwa mchezo wao na Timu
ya Jamuhuri uliofanyika Uwanja wa Amaan usiku,
Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri wakisalimiana na Wachezaji wa Timu ya
Yanga kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la
Mapinduzi Cup uliofanyika Uwanja wa Amaan Usiku.
Kikosi cha Timu ya Yanga African kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi Cup
kilichoaza michuano hiyo kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Timu ya
Jamuhuri kutoka Kisiwani Pemba mchezo uliofanyika uwanja wa amaan
Zanzibar usiku.
Kikosi cha Timu ya Jamuhuri kutoka Pemba kinashoririki Michuano ya Kombe
la Mapinduzi CUP kilichokubali kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Timu ya
Yanga African.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga African Msuva akijaribu kumpita beki wa
Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika
usiku katika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Yanga Afrika imeshinda kwa
mabao 6-0.
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakishangilia bao lao la kwanza.katika mchezo
wa Kombe la Mapinduzi Cup mchezo uliofanyika usiku uwanja wa amaan
Zanzibar.
Golikipa wa Timu ya Jamuhuri akiwa na majozi baada kufungwa bao la sita
na timu ya yanga wakati wa mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi
Cup mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amaan Zanzibar usiku.
0 comments:
Post a Comment