Tuesday, January 10, 2017

 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
CHINA imesema, itajenga viwanda kuunga mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo Januari 9, 2017, na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Bw. Wang Yi, (pichani juu, alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa, kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo ambaye amewasili leo mchana akitokea nchini Zambia, alimuhakikishia waziri mkuu azma ya serikali ya China, kujenga ushirikiano wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili. Ziara ya Waziri huyo ambayo ni ya kufungua msimu mpya wa mwaka 2017 wa uhusioano baina ya China na mataifa ya Kiafrika, inalenga kuweka msisitizo wa ahadi alizotoa Rais wa China, alipotembelea Tanzania mwishoni mwa mwaka jana.
Baadaye waziri huyo na ujumbe wake, walikutana na kufanya mazunhumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mmabo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere.

 Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa, (kulia), akiwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa China, Bw. Wang Yi, (wapili kulia), nyumbani kwake Oyseterbay jijini Dar es Salaam, Januari 9, 2016. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Waziri Wang na ujumbe wake (kushoto), wakifanya mazungumzo ya kiserikali na mwenyeji wake na Dkt. Augustine Mahiga na ujumbe wake kulia, kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Waziri Wanga, na mwenyeji wake, Dkt. Augustine Mahiga, wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya kiserikali
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
 Waziri Wanga Yi, na mwenyeji wake, Dkt. Mahiga, wakipiga picha rasmi
 Waziri Wanga na mwenyeji wake, katika mkutano na wanahabari
 Waziri Wanga, na mwenyeji wake, Waziri Dkt. Mahiga, wakitoka kwenye mkutano na wanahabari
 Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Dkt. LU Youqing
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya serikali wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (kushoto), akiongoza mkutano na waandishi wa habari, uliohutubiwa na Mawaziri Wanga, na Balozi Dkt. Mahiga

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu