Thursday, January 19, 2017

CHINA YA JIANEXI-GEO ENGINEERING GROUP CORPORATION YAKABIDHI SAMANI ZA OFISI KWA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu namna Wizara yake ilivyopokea kwa furaha vifaa hivyo na jinsi gani imejipanga kuvitumia katika kuhakikisha kuwa inawahudumia Wananchi kwa kuwapa huduma bora. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei. Makabidhiano hayo yamefanyika leo 19/0/2017 katika Ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua (kulia) pamoja na Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Waandishi wa habari kabla ya hafla ya makabidhiano ya samani za ofisi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na Maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati akiishukuru Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation kwa msaada wa samani za ofisi iliyoutoa kwa Wizara hiyo leo 19/01/2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua (kulia)
akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Kampuni yake ya kushirikiana na Serikali katika kusaidia kuleta maendeleo kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Sekta ya Sanaa na Utamaduni. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei, leo 19/0/2017 Jijini Dar es Salaam.


Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Kampuni Jianexi-Geo Engineering Group Corporation pamoja Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China ya kushirikiana na Serikali katika kusaidia kuleta maendeleo kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Sekta ya Sanaa na Utamaduni. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei, leo 19/0/2017 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi (kushoto) pamoja Afisa Utamaduni (Kitengo cha Sanaa) Bi. Amney Kassam wakichukua taarifa za aina ya samani walizopokea kutoka kwa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani za ofisi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akipokea moja ya samani za ofisi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakiweka saini Hati za Makabidhiano ya Samani za ofisi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakibadilishana Hati za Makabidhiano ya Samani za ofisi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.
 (Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu