Tuesday, January 31, 2017

JUMIA TRAVEL YAJIKITA KATIKA UTALII


Na Jumia Travel Tanzania

Mwaka wa 2016 ulikuwa wenye mafanikio makubwa kwa sekta ya utalii duniani ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), watu bilioni 1.2 walisafiri duniani huku waliotembelea Afrika wakiwa milioni 58.


Taarifa hiyo ilitolewa katika mkutano wa nane uliondaliwa wa INVESTOUR Januari 19, 2017 jijini Madrid nchini Hispania, kwa ushirikiano wa UNWTO na Casa Afrika ambao uliwakutanisha wadau na mawaziri zaidi ya 20 wa utalii kutoka barani Afrika.   

Ajenda kuu za mkutano huo zilikuwa mbili ambazo ni; ‘Tekinolojia na uundaji wa bidhaa mpya za kitalii’ pamoja na ‘Kuendeleza uwezo kwa vijana na wanawake katika utalii.’

Akiwa na mmojawapo wa washiriki waliounda jopo la wazungumzaji katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy alibainisha kwamba, “Idadi kubwa ya wasafiri wa ndani ni ishara nzuri kwamba watu wanavutiwa na vivutio walivyonavyo. Zinahitajika jitihada za wadau wa utalii katika kuwaelimisha na kuvitangaza vivutio hivyo huku tukiwarahisishia miundombinu kama vile malazi ambayo huwezi kuiweka kando pindi unapozungumiza usafiri na utalii. Naamini kwa gharama za malazi kupunguzwa, watu wengi watahamasika kusafiri kwani mahali zilipo hizo hoteli ndipo vivutio vilipo.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna fursa kubwa kwa utalii wa ndani kwa sababu mbali na idadi ya watu bilioni 1.2 waliosafiri duniani, watu bilioni 6 walifanya utalii wa ndani. Hii inamaanisha kwamba zinahitajika kufanyika jitihada za makusudi katika kuhamasisha na kutangaza vivutio vya nyumbani ili kuwavutia watu wengi zaidi.   

Katika kulifanikisha hilo Jumia Travel imekuwa ikitoa punguzo kubwa la bei kila ifikapo siku ya Jumatano na kudumu mpaka siku ya Ijumaa kila wiki. Ofa hii hutoa fursa na kuwarahisishia watu wanaotamani kwenda kutalii sehemu fulani lakini wakihofia bei ya malazi kuwa juu.

Hoteli zote ambazo zimo kwenye orodha ya ofa hii zinapatikana kwenye maeneo ambayo yana vivutio vya kitalii kama vile mbuga za wanyama, milima, fukwe safi na za kuvutia za bahari, ndege wa kuvutia pamoja na vyakula na utamaduni wa eneo husika.  


Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu