Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
07/10/2017
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
07/10/2017
Serikali imewaagiza
wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia
hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi
haramu.
Akizungumza baada ya
kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba za Maliasili, Ulinzi, Nishati na
Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya Ndani Naibu Waziri
TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia agenda ya kupambana na
uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu katika
vikao vyao.
Alisema kuwa maafisa uvuvi
hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia ni kiasi gani
wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia mabomu.
“Kuna baadhi ya mafisa uvuvi
wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho wataanza
kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa katika
nyazifa hiyo”.
Kwa upande wake Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema kuwa nchi yetu
inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya
uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika
kupambana na uharamia huo.
Akifafanua zaidi kuhusu
hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa jambo la
uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi wa nchi hivyo
lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa.
Alisema ni aibu kwa
taifa letu la Tanzania kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi nyingi kwa
sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.
Naye Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania wote kushirikiana na Serikali
katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi haramu.
Mwigulu Nchemba
alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika kulinda
rasilimali za majini tulizo nazo”.
Kikao hicho ni
utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu ambapo
maazimio hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita kwa
ajili ya kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale
patakapoonekana pana changamoto

0 comments:
Post a Comment