Tuesday, January 24, 2017


Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds cha kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab(wapili kushoto) akimuonyesha Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe zilizotengenezwa kitalaam na kuhifadhiwa kwenye mifuko maalumu tayari kwa kuuzwa sokoni,wakati alipotembelea Kikundi hicho hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hichokilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.


Wakinamama wa kikundi cha 2Seeds, wa  kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga,wakishirikiana na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa  Vodacom  Tanzania Foundation,Sandra Oswald (wapili kulia) kumenya viazi  wakati alipotembelea kikundi hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi  mbalimbali ya ujasiliamali,ufugaji, Kilimo,inayofanywa na kikundi hicho na kufadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.


Bibi  Masoko wa kikundi cha 2 Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga ,Mariam Jecha (wapili kulia) akimfafanulia jambo hivi karibuni,Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald (Kushoto) kuhusiana na jiko la kisasa la kukaangia chips za viazi na mihogo zinazozalishwa na kikundi hicho  baada ya kupata mafunzo  ya ujasiliamali kutoka kwenye taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds  ya nchini Marekani  yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo umefadhiliwa na na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation”


Mratibu wa kikundi cha 2Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga, Moshi Abdallah(kushoto)  akimuonyesha mradi wa kilimo cha mboga Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.



Moshi Abdallah na Monica Ayubu wa kikundi cha 2Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga,wakimshuhudia  Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald,(kulia) akiangalia ubora wa vyakula vinavyosindikwa na kikundi hicho, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu