Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na
Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akizungumza na waandishi
wa habari wakati walipotembelea shamba la utafiti wa zabibu katika Kituo
cha Utafiti wa Kilimo Makutupora mkoani Dodoma leo.
safari kuelekea shamba la zabibu ikiendelea.
Mkurugenzi wa
Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (katikati),
akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zabibu kwa wanahabari. Kushoto Mtafiti
Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle na kulia ni Mtafiti Andekelile
Mwamahonje.
Wanahabari wakiwa katika shamba hilo.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akionesha mche wa zabibu uliostawi vizuri.
Wanahabari wakiangalia shamba hilo.
Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zao la zabibu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) |
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
VIJANA wametakiwa wajiunge kwenye
vikundi na kuanzisha mashamba ya kilimo cha zabibu ili wajipatie kipato
badala ya kukaa vijiweni.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa
Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso wakati
akizungumza na wanahabari waliotembelea shamba la zabibu katika Kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.
"Mwito wangu kwa vijana waanzishe
vikundi vitakavyoweza kuwasaidia kuanzisha mashamba ya zabibu ili
wajiongezee kipato mikopo ya kuwezeshwa ipo" alisema Mroso.
Alisema mtaji wa kuanzisha shamba la
zabibu ni kuanzia sh. milioni tatu hadi nne ambapo baada ya miaka mitatu
au minne mkulima anaanza kunufaika na kilimo hicho.
Alisema katika kuinua pato la taifa na
la mtu mmoja mmoja serikali imeaanzisha mashamba ya zabibu maeneo
mbalimbali mkoani humo ambapo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino
kuna shamba la ekari 296, katika Kijiji cha Kamaiti wilayani Bahi kuna
shamba la ekari 170 na Manispaa ya Dodoma katika Kijiji cha Gawaye kuna
ekari 100 ambapo kila mwananchi hasa vijana wamepatiwa ekari moja
kuziendeleza.
Alitaja aina za zabibu zinazolimwa
katika maeneo hayo kuwa ni za mezani, mvinyo na kukausha ambazo soko
lake linapatikana wakati wote.
0 comments:
Post a Comment