2


SI LA KULIKOSA

Monday, February 20, 2017


Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Kagera  ikiwa na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya. Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari 19, 2017  wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho  kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli  ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho.


Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017.Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
MZUKA BLOG © Copyright 2014. All Rights Reserved.

Powered by MATERU FROM IBS.
imagem-logoRudi Juu